Loading...
title : HOPE FOR ALL YAWATAKA VIJANA KUTOBWETEKA, WAKOME KUSUBIRI URITHI WA MALI ZA WAZAZI
link : HOPE FOR ALL YAWATAKA VIJANA KUTOBWETEKA, WAKOME KUSUBIRI URITHI WA MALI ZA WAZAZI
HOPE FOR ALL YAWATAKA VIJANA KUTOBWETEKA, WAKOME KUSUBIRI URITHI WA MALI ZA WAZAZI
Na Richard Mwaikenda-Dar .
WANAFUNZI waliomaliza Kidato cha Nne, wametakiwa kuachana na tabia ya kupoteza muda kusubiri kurithi mali za wazazi wao, bali wajitambue kwa kufanya kazi kwa bidii kujiletea maendeleo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All , Edger Mwamfupe wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kujitambua wanafunzi waliomaliza Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Makongo Juu, Dar es Salaam hivi karibuni.
“Kila mmoja ajitambue kivyake,, simama wewe kama wewe, jitambue wewe ni nani, ukijiami kama unaweza na utaweza kweli. Mkome kutegemea kurithi mali za baba zenu,” aliwaaasa Mwamfupe.
“Msiruhusu ndoto zenu zife, hata kama mtakumbana na mazingira magumu majumbani kwenu, mzishikile msiruhusu ndoto zenu zife, Kawaida wewe ndiyo unaamua kuwa tajiri au masikini , utajiri uko kichwani kwako,” alisisitiza Mwamfupe huku akipigiwa makofi na wanafunzi.
Mwamfupe, hakusita kujitolea mfano yeye kuhusu maisha yake ya ujana, ambapo aliwaeleza kuwa licha ya utajiri wa babake, lakini yeye aliamua kujitegemea tangu akiwa anasoma na kwamba alipokuwa ana miaka 19 alinunua gari aina ya Toyota Corola (Mayai).Pia, kupitia kipaji chake cha kucheza mpira na ngoma za asili kilifanya kwa mara ya kwanza apande ndege kwenda Romania kuiiwakilisha Taifa katika Tamasha la Ngoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All , Edger Mwamfupe (Kulia), akimsikiliza mmoja wa wanafunzi aliyekuwa akijieleza jinsi atakavyokabiliana na maisha baada ya kumaliza shule..
Wanafunzi wakisikiliza kwa makini wakati wa mafunzo hayo
Mkuu wa Kitengo cha Vijana cha Taasisi hiyo, Harrison Edger akiwa tia moyo wanafunzi hao.
Hivyo makala HOPE FOR ALL YAWATAKA VIJANA KUTOBWETEKA, WAKOME KUSUBIRI URITHI WA MALI ZA WAZAZI
yaani makala yote HOPE FOR ALL YAWATAKA VIJANA KUTOBWETEKA, WAKOME KUSUBIRI URITHI WA MALI ZA WAZAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HOPE FOR ALL YAWATAKA VIJANA KUTOBWETEKA, WAKOME KUSUBIRI URITHI WA MALI ZA WAZAZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/hope-for-all-yawataka-vijana.html
0 Response to "HOPE FOR ALL YAWATAKA VIJANA KUTOBWETEKA, WAKOME KUSUBIRI URITHI WA MALI ZA WAZAZI"
Post a Comment