Loading...

KILUWA AFANIKIWA KUWAHAMASISHA WACHINA KUJA NCHINI TANZANIA KUJENGA VIWANDA VITATU MLANDIZI

Loading...
KILUWA AFANIKIWA KUWAHAMASISHA WACHINA KUJA NCHINI TANZANIA KUJENGA VIWANDA VITATU MLANDIZI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KILUWA AFANIKIWA KUWAHAMASISHA WACHINA KUJA NCHINI TANZANIA KUJENGA VIWANDA VITATU MLANDIZI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KILUWA AFANIKIWA KUWAHAMASISHA WACHINA KUJA NCHINI TANZANIA KUJENGA VIWANDA VITATU MLANDIZI
link : KILUWA AFANIKIWA KUWAHAMASISHA WACHINA KUJA NCHINI TANZANIA KUJENGA VIWANDA VITATU MLANDIZI

soma pia


KILUWA AFANIKIWA KUWAHAMASISHA WACHINA KUJA NCHINI TANZANIA KUJENGA VIWANDA VITATU MLANDIZI

*Dola za Marekani milioni 100 kutumika katika ujenzi 
*Ahimiza Watanzania kuwa wazalendo kwa nchi yao

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MWENYEKITI wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd Mohammed Kiluwa amesema katika kuhakikisha anaunga mkono jitihada za Rais Dk.John Magufuli za ujenzi wa Tanzania ya viwanda amefanikiwa kuwashawishi wawekezaji kutoka nchini China kuja kujenga viwanda kuwekeza nchini.

Kiluwa amesema kupitia ushawishi wake na kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) wawekezaji hao kutoka China wamekubali kujenga kiwanda cha kuongeza thamani ya bidhaa za ngozi, Kiwanda cha Saa pamoja na Kiwanda cha Simu na kwamba awamu ya kwanza ya uwekezaji huo jumla ya dola za Marekani milioni 100 zitatumika.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu ujio wa wawekezaji hao Kiluwa amesema viwanda hivyo vitajengwa Mlandizi mkoani Pwani na wakati wowote kuanzia sasa baada ya kukamilisha taratibu zote ikiwemo za vibali ujenzi wa viwanda hivyo utaanza mara moja.Pia amesema mbali ya kujengwa kwa viwanda hivyo wawakezaji hao wameonesha nia ya kujenga kiwanda cha kubangua korosho mkoani 

Mtwara na kinachoendelea sasa ni mazungumzo ambayo yanakwenda vizuri na hakuna kitakachoshindikana."Wawekezaji hawa wameonesha nia kujenga kiwanda cha korosho na walikuwa tayari kwenda mkoani Mtwara kuona mazingira." 

Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. John Mathew Mnali akizungumza jambo mbele ya waandishi wa Habari leo jijini Dar kuhusu masuala mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda,ikiwemo na kuwapokea wageni wa uwekezaji wa viwanda kutoka nchini China na wenyeji wao kutoka kampuni ya Kiluwa Group Ltd.


MWENYEKITI wa Makampuni ya Kiluwa Group Ltd Mohammed Kiluwa (pichani kushoto) akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari leo alipokwenda kuwatambulisha Wadau wake wa Uwekezaji katika masuala ya Viwanda kutoka nchini China,kwa kituo cha Uwekezaji nchini (TIC),na kueleza mikakati yao mbalimbali waliyonayo kuhusiana na uwekezaji wa viwanda nchini Tanzania,kulia ni Mkurugenzi wa Kukuza Uwekezaji kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bw. John Mathew Mnali. 

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe akisalimia na Mkurugenzi wa kampuni ya Kiluwa Group,Naima Mohamed Kiluwa,walipokwenda kwenye ofisi za kituo hicho kuwatambulisha wadau wao wa uwekezaji katika mambo ya Uwekezaji wa Viwanda,anaeshuhudia pichani kati Mwenyekiti wa Kampuni ya Kiluwa Group,Mohamed Kiluwa (pichani kati) na kuwasilisha mikakati yao mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yinengda New Material Techonology Mayi Hong alipokuwa akifafanua jambo kuhusiana na mambo ya uwekezaji wa viwanda hapa nchini Tanzania,maara aada kuzungumza na waandishi wa habara katika ofisi za kituo hicho .
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yinengda New Material Techonology Mayi Hong akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC),Geofrey Mwambe walipowasili leo kwenda kutambulishwa na Mdau wake Mkubwa kwenye mambo ya Uwekezaji wa Viwanda,Mwenyekiti wa Kampuni ya Kiluwa Group,Mohamed Kiluwa (pichani kati) na kuwasilisha mikakati yao mbalimbali ya uwekezaji wa viwanda. 


KUSOMA ZAIDI BOFYA  HAPA>>>


Hivyo makala KILUWA AFANIKIWA KUWAHAMASISHA WACHINA KUJA NCHINI TANZANIA KUJENGA VIWANDA VITATU MLANDIZI

yaani makala yote KILUWA AFANIKIWA KUWAHAMASISHA WACHINA KUJA NCHINI TANZANIA KUJENGA VIWANDA VITATU MLANDIZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KILUWA AFANIKIWA KUWAHAMASISHA WACHINA KUJA NCHINI TANZANIA KUJENGA VIWANDA VITATU MLANDIZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/kiluwa-afanikiwa-kuwahamasisha-wachina.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KILUWA AFANIKIWA KUWAHAMASISHA WACHINA KUJA NCHINI TANZANIA KUJENGA VIWANDA VITATU MLANDIZI"

Post a Comment

Loading...