Loading...

MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA

Loading...
MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA
link : MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA

soma pia


MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kwa kila Mkuu wa Mkoa aifanye afya ya uzazi na mtoto kuwa ajenda ya kudumu katika vikao vya ushauri vya Mkoa (RCC).

Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo leo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya “Jiongeze Tuwavushe Salama” ya Kuongeza kasi ya Uwajibikaji Kupunguza Vifo Vitokanavyo na Uzazi na Watoto Wachanga.

“Ili kuhakikisha suala la kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto katika nchi yetu linapewa kipaumbele cha juu katika shughuli za Serikali za kila siku” alisema Makamu wa Rais

Tafiti zilizofanyika mwaka 2015/2016 zinaonyesha kuwa, kiwango cha vifo vitokanavyo na uzazi ni 556 kwa kila vizazi hai 100,000 ambayo ni sawa na vifo 11,000 kila mwaka ambayo ni sawa na wanawake 30 hufariki kila siku, kutokana na matatizo yatokanayo na uzazi na kwa uapnde wa watoto wachanga ni 25 kwa kila vizazi hai 1000 .

Makamu wa Rais amesema jamii ina jukumu zito la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kwa kuhakikisha kuwa inajiwekea mpango mahsusi wa rufaa wakati wa dharura na utambuzi wa dalili hatarishi kwa mama na mtoto mchanga.

“Nitoe rai kwa wananchi, wanawake na wanaume na vijana kujitokeza kuchangia damu mara kwa mara kwa kuwa wakifanya hivi wanaokoa maisha ya mama mjamzito na watoto.” Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 80 ya damu salama inatumika kwa wakina mama wajawazito na watoto alisema Makamu wa Rais.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" jijini Dodoma.wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" jijini Dodoma.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akionesha taarifa inavyoonyesha hali halisi ilivyo sasa katika masuala yanayohusu uzazi salama wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" jijini Dodoma.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia wakati wa uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.
 Sehemu ya Wageni kutoka Taasisi mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kampeni ya "Jiongeze Tuwavushe Salama" ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Hazina jijini Dodoma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA

yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/makamu-wa-rais-azindua-kampeni-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAKAMU WA RAIS AZINDUA KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA"

Post a Comment

Loading...