Loading...
title : MANYANYA AZIAGIZA TAASISI ZA UDHIBITI WA BIDHAA,CHAKULA NA DAWA NCHINI KUWA KARIBU NA WAJASIRIAMALI
link : MANYANYA AZIAGIZA TAASISI ZA UDHIBITI WA BIDHAA,CHAKULA NA DAWA NCHINI KUWA KARIBU NA WAJASIRIAMALI
MANYANYA AZIAGIZA TAASISI ZA UDHIBITI WA BIDHAA,CHAKULA NA DAWA NCHINI KUWA KARIBU NA WAJASIRIAMALI
NAIBU Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya ameziagiza taasisi za udhibiti wa bidhaa,chakula na dawa nchini kuhakikisha zinakuwa karibu na wajasiriaamali ili kuweza kuwasaidia badala ya kuwakamata kwa kigezo cha kutokufanya vizuri.
Hayo ameyazungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Kanda ya Kaskazini ya SIDO alipokuwa akiwahutubia wajasiriamali hao na kusema wataalamu wa taasisi hizo wanapaswa kutoa elimu ya kuwajengea uwezo badala ya kutoza faini.
Aidha alisema wajasiaramali wengi nchini hasa wadogowadogo bado hawajakuwa na uwelewa mpana wa namna ya kuweka mpangilio mzuri wa maswala mazima ya shughuli zao hivyo wanahitaji kuelimishwa. “Tunao wataalamu toka TBS,TFDA na taasisi nyingine za udhibiti lakini wanatakiwa kuelimisha zaidi badala ya kuwafungia baadhi ya wajasiriamali au kuwatoza faini na haya sio malengo ya Serikali”Alisema Manyanya.
Manyanya alisema lengo la Serikali hadi kufikia 2025 kufikia katika uchumi wa viwanda jambo ambalo linahitaji nguvu ya ziada ikiwa pamoja na kuwaelimisha wajasiriamali hao na kuwawezesha kimitaji. Hata hivyo aliwataka wajasiriamali wote Nchini kuhakikisha wanaimarisha ubora wa viwango wa bidhaa zao wanazozalisha ili kuendana na ushindani wa soko na kuongeza ubunifu ili waweze kuuza katika nchi za Afrika Mashariki.
Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya akizungumza wakati akifungua maonyesho SIDO ya Kanda ya Kaskazini yanayoendelea kwenye viwanja vya Tangamano mjini Tanga kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Joyce Meru
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Joyce Meru akizungumza katika ufunguzi huo
Naibu Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Stella Manyanya kulia akipata maelezo kutoka kwa Banda la Tanga Fresh.
Hivyo makala MANYANYA AZIAGIZA TAASISI ZA UDHIBITI WA BIDHAA,CHAKULA NA DAWA NCHINI KUWA KARIBU NA WAJASIRIAMALI
yaani makala yote MANYANYA AZIAGIZA TAASISI ZA UDHIBITI WA BIDHAA,CHAKULA NA DAWA NCHINI KUWA KARIBU NA WAJASIRIAMALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MANYANYA AZIAGIZA TAASISI ZA UDHIBITI WA BIDHAA,CHAKULA NA DAWA NCHINI KUWA KARIBU NA WAJASIRIAMALI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/manyanya-aziagiza-taasisi-za-udhibiti.html
0 Response to "MANYANYA AZIAGIZA TAASISI ZA UDHIBITI WA BIDHAA,CHAKULA NA DAWA NCHINI KUWA KARIBU NA WAJASIRIAMALI"
Post a Comment