Loading...
title : MHANDISI NYAMHANGA: HAKUNA SABABU ZA KUCHELEWESHA MRADI
link : MHANDISI NYAMHANGA: HAKUNA SABABU ZA KUCHELEWESHA MRADI
MHANDISI NYAMHANGA: HAKUNA SABABU ZA KUCHELEWESHA MRADI
Serikali imewataka Makandarasi wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Tabora-Koga-Mpanda yenye urefu wa KM 359 inayounganisha Mkoa wa Tabora na Katavi kupitia daraja la Koga, kufanya kazi kwa bidii ili kukamilisha mradi huo kabla ya muda uliopangwa.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph nyamhanga, wakati wa ziara yake katika mikoa hiyo ambapo amesema fedha za mradi huo zipo hivyo hakuna sababu ya kuuchelewesha. "Fedha za ujenzi wa mradi huu zipo hivyo fanyeni kazi usiku na mchana ili kukamilisha mapema barabara hii kwani hakuna vikwazo vyovyote na mvua isiwe sababu ya kusimamisha kazi za ujenzi", amesema Mhandisi Nyamhanga.
Mhandisi Nyamhanga, amewataka wasimamizi wa mradi wakishirikiana na Mameneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), wa mikoa hiyo kusimamia mradi huo kwa ukamilifu na kwa ubora uliopangwa bila kuongeza gharama. "Hakikisheni mradi huu unasimamiwa kwa ubora uliopangwa na mdhibiti gharama za mradi hata ikiwezekana ipatikane akiba ya fedha ambayo itatumika kwa miradi mingine ya barabara hapa nchini", amesisitiza Katibu Mkuu huyo.
Ameeleza umuhimu wa kukamilika kwa barabara hiyo kuwa utakuza uchumi wa wananchi na kuongezeka kwa shughuli za kibiashara kwakuwa ni miongoni mwa mikoa yenye uzalishaji mwingi wa bidhaa mbalimbali za kilimo, ufugaji wa nyuki, madini na utalii. Kuhusu uharibifu wa miundombinu ya barabara hapa nchini, Mhandisi Nyamhanga, ametoa wito kwa wananchi wa mikoa hiyo kuilinda miundombinu hiyo kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekamatwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akikagua kingo za daraja la kasisi katika barabara ya Tabora-Sikonge yenye urefu wa KM 30 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
Mkandarasi wa kampuni ya M/S Jiangxi Geo-Engineering, Li Jinaru, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, wakati alipokagua mitambo ya kuchanganya lami katika kambi ya mkandarasi huyo anayejenga barabara ya Usesula-Komanga yenye urefu wa KM 108 kwa kiwango cha lami, Mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya LEA International Bw. Sanjeev Gupta (wa tatu kushoto) anayesimamia ujenzi wa barabara ya Usesula-Komanga yenye urefu wa KM 108, kwa kiwango cha lami, wakati akikagua hatua za ujenzi wa barabara hiyo, mkoani Tabora.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Tabora-Sikonge yenye urefu wa KM 30, iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MHANDISI NYAMHANGA: HAKUNA SABABU ZA KUCHELEWESHA MRADI
yaani makala yote MHANDISI NYAMHANGA: HAKUNA SABABU ZA KUCHELEWESHA MRADI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MHANDISI NYAMHANGA: HAKUNA SABABU ZA KUCHELEWESHA MRADI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/mhandisi-nyamhanga-hakuna-sababu-za.html
0 Response to "MHANDISI NYAMHANGA: HAKUNA SABABU ZA KUCHELEWESHA MRADI"
Post a Comment