Loading...
title : MSAJILI WA NGOs ATEMA CHECHE, AZITAKA NGOs KUWAJIBIKA KWA WANANCHI
link : MSAJILI WA NGOs ATEMA CHECHE, AZITAKA NGOs KUWAJIBIKA KWA WANANCHI
MSAJILI WA NGOs ATEMA CHECHE, AZITAKA NGOs KUWAJIBIKA KWA WANANCHI
Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga ameyataka Mashirika hayo kuwajibika kwa wananchi kwa kuhakikisha wanatekeleza miradi wanayoiombea fedha kwa kushirikiana na Serikali.
Ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati alipokutana na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani humo kwa lengo la kujitambulisha, kujadiliana na kujua changamoto zinazoyakabili Mashirika hayo katika kutekeleza majukumu yake.
Bi. Neema amesema kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanatakiwa kujiendesha kwa kuzingatia Sheria na taratibu za nchini na kuwa wazi, kuwajibika ila baadhi ya NGOs zimekuwa zikifanya kazi bila kuzingatia uwazi na uwajibikaji hivyo kupeleka upotevu wa rasilimali zilizoombwa kwa lengo la kuwaletea watanzania maendeleo.
Ameongeza kuwa lengo la mkutano huo na wadau wa NGOs mkoani Arusha ni kujadiliana na kupata namna bora za kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya NGOs nchini na kusema kuwa ana imani mkutano huo utatoka na majibu sahihi yatakayowezesha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Arusha kutekeleza majukumu yake katika misingi ya uwazi na uwajibikaji.
Msajili huyo amesisitiza kuwa Serikali inatambua mchango wa Mshirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kuwa inatoa ajira kwa watanzania na kusaidiana na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo kupitia Miradi mbalimbali katika Sekta za Afya, Mazingira na Kilimo na Sekta nyingine hivyo kuchangia katika kusogeza mbele gurudumu la maendeleo la taifa.
Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga akizungumza na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Arusha katika ziara yake ya kutembelea wadau hao, kutambua changamoto zao na kutoa maelekezo ya uzingatiaji wa sheria, kanuni na taratibu za usimamizi wa fedha na uendeshaji wa miradi yao katika ngazi ya jamii.
Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Utaratibu mkoa wa Arusha Bw. Moses Mabula akielezea namna Serikali ya mkoa unavyoratibu na kuyasimamia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ngazi ya Mkoa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha wakati wa ziara ya Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga mkoani humo.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Baraka Leonard akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wa mkoa wa Arusha kushoto ni Msajili na Mkurugenzi wa Idara ya Usajili na Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga na katikati ni Katibu Mkuu wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCONGO) Bw. Ismail Suleiman.
Mwakilishi wa Shirika la the Girls Foundation of Tanzania Bi. Esther Happy Mariki akiuliza swali kwa Msajili wa NGOs katika kikao kilichowakutanisha Wadau wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Arisha na Msajili wa NGOs wakati wa Ziara ya Msajili huyo kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Neema Mwanga mkoani humo
Baadhi ya wawakilishi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali mkoani Arusha wakimsikiliza Msajili wa NGOs Bi. Neema Mwanga (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Msajili huyo mkoani humo kujitambulisha na kutambua changamoto za mashirika hayo nchini ili kukuza uwazi na uwajibikaji. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Hivyo makala MSAJILI WA NGOs ATEMA CHECHE, AZITAKA NGOs KUWAJIBIKA KWA WANANCHI
yaani makala yote MSAJILI WA NGOs ATEMA CHECHE, AZITAKA NGOs KUWAJIBIKA KWA WANANCHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MSAJILI WA NGOs ATEMA CHECHE, AZITAKA NGOs KUWAJIBIKA KWA WANANCHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/msajili-wa-ngos-atema-cheche-azitaka.html
0 Response to "MSAJILI WA NGOs ATEMA CHECHE, AZITAKA NGOs KUWAJIBIKA KWA WANANCHI"
Post a Comment