Loading...
title : Mtoto aliouawa kwa kipigo cha mama yake azikwa na mamia Babati
link : Mtoto aliouawa kwa kipigo cha mama yake azikwa na mamia Babati
Mtoto aliouawa kwa kipigo cha mama yake azikwa na mamia Babati

Na John Walter,BABATI
JESHI la Polisi Mkoani Manyara linamshikilia Mariamu Daudi [40] mkazi wa wa mtaa wa Komoto Babati mjini kwa tuhuma za kumuua mtoto wake Emmanuel Justine [11] mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kwang’w huku likimsaka kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Amani ambaye alishirikiana na mama huyo.
Akizungumza kamanda wa polisi mkoani hapa Augustino Senga alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na mpaka sasa wanamshikilia mama mzazi wa mtoto huyo kwa mahojiano zaidi.
Aidha kamanda Senga alisema mtoto huyo alidaiwa kuiba nyiwa kwa Aman ambaye anasakwa na polisi na mtuhumiwa anayesakwa alimshambulia mwanafunzi huyo kwa kumpiga fimbo huku akiwa amesimamiwa na mama yake mzazi wa mtoto aliyeuliwa.
“Taarifa tulizopata kijana aliyefanya unyama huo anajulikana mitaani hivyo tunaendelea kufanya upelelezi na tukimkamata hatua zingine zitaendelea za kuwafikisha watuhumiwa mahakamani kwa ajili ya kujibu mashtaka,’’Alisema Senga
Alitumia fursa hiyo kuitaka jamii kuwalea watoto katika maadili mazuri na kuepuka kutoa adhabu ambazo zimezidi kipimo kwa watoto kwa kua kufanya hivyo ni kuvunja sheria za nchi na wanaokiuka serikali lazima iwachukulie hatua.
Mmoja wa majirani waliosaidia kumnusuru mtoto huyo Stela Michael alisema mama yake aliwaambia mtoto huyo amezidi utukutu hivyo amechoka kuletewa mashitaka nyumbani kwake lakini anasema mama huyo adhabu aliyompa mtoto ilipitiliza kuzidi uwezo.
“Mimi niliitwa na mtoto mwenzake aliyedaiwa kua walichapwa pamoja akisema Emma ananiita baada ya kufika nilimkuta mtoto anagalagala chini ameishiwa na nguvu na mama yake akaja tukasaidiana kumpa uji aliposikia mama yake aligoma kunywa lakini nilipomnywesha mimi na akasikia sauti yangu alikubali akanywa mara moja na kuishiwa nguvu ndio walimpeleka Hospitali,’’Alisema jirani huyo.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa Komoto Paschal Hondi alisema matukio ya ukatili katika mtaa huo yamekuwa ni endelevu na baba yake na mtoto huyo alisema marehemu amekufa ghafla nay eye anadai hakuwepo nyumbani wakati mauti yanamkuta mwanae.
Aliongeza kua msiba huo wao wameupokea kwa masikitiko makubwa maana umeigusa jamii na matukio ya namna hiyo ya kikatili yanaendelea kujitokeza katika mtaa huo licha ya serikali kupiga kelele dhidi ya ukatili.
Kwa upande wake Justine Mkilanyi ambaye ni baba wa mtoto aliyeuwawa alisema mtoto wake alienda shuleni siku ya ijumaa akiwa mzima na baadaye alirejea na kusema kua walimu wamemrudisha nyumbani kua aende na baba yake shuleni jambo ambalo Mkilanyi akuridhia maana alikua anawahi kazini na akamuambia aende na mama yake.
“Ndipo walienda na mama yake na akaambiwa na walimu kua mtoto wake ni mtukutu ambapo waliulizwa wanafunzi wa darasani kwake kua nani aliwahi kupigwa na Emmanuel ndio darasa zima liliamka,’’Alisema Mkilanyi.
Alifafanua kua mke wake aliambiwa arudi nyumbani na mtoto wake na aliporudi na mtoto huyo walimkuta baba huyo bado yupo nyumbani na mtoto wake alimwambia kua amefukuzwa na alimlalamikia kuwa alishamwambia amuhamishe shule hiyo toka yuko darasa la kwanza kumpeleka shule ya binafsi.
“Mimi nilimuomba avumilie nije nimpeleke shule hiyo nitakua ninalipa kidogo kidogo ila aliniambia baba ninaondoka sasa ndipo nikaenda kazini niliporudi jioni sikumkuta nikamtafuta mpaka saa nne usiku sikumpata kesho yake nikapata taarifa alilala kwa ndugu yangu,’’Alisema Mkilanyi
Aidha alisema kesho yake alipoenda kazini kurudi nyumbani alikuta mauti yamemkuta na watu wamejaa nyumbani kwake, wakati huo aliiambia Nipashe kua huyo mtoto ndio alimpenda sana maana alikkua anaweza kufanya kazi za ufundi, ufugaji na uchoraji kama baba yake ambaye anaona angemrithi.
Kituo hiki kilizungumza na mwalimu wa darasa wa mwanafunzi huyo Emmanuel na kumuuliza kama kweli mtoto huyo walimshindwa walimu na kumrudisha nyumbani kwa muda usiojulikana lakini mwalimu Nuru Belshaza alikana kumrudisha nyumbani mwanafunzi huyo huku akisema wao hawawezi kumshindwa mwanafunzi.
Katika hali ya kusikitisha juu ya tukio hilo mashuhuda wengi waliozungumza kwa sharti la kutokuandikwa walisema mama wa mtoto huyo alishirikiana na Amani kumcharaza kwa kutumia fimbo ya mbaazi huku mama yake akitumia mpini na wengine wakidai walimfunga mikono na miguu na kuanza kumtembezea kichapo bila huruma licha ya mwanafunzi huyo kupiga kelele kuomba msamaha.
Wengine waliongeza kuwa mama huyo alimlipatia shilingi elfu kumi [10,000] ili kijana huyo amsaidie kumkimbiza mtoto huyo na waweze kumpa adhabu ili abadilike maana alikuwa ni kero nyumbani na mitaani kwa baadhi ya watu.
Mwinjilisti Raymond Francis aliyeendesha ibada ya mazishi ya mwanafunzi huyo aliwaambia waombolezaji kuwa tukio hilo ni la kinyama hivyo wawe wanatoa adhabu yenye kipimo ambayo haitageuka kuwa chukizo kwa Mungu maana inaweza kumfanya mtoa adhabu aonekane ametoa hukumu wakati kazi ya hukumu ni ya Mungu peke yake.
Hivyo makala Mtoto aliouawa kwa kipigo cha mama yake azikwa na mamia Babati
yaani makala yote Mtoto aliouawa kwa kipigo cha mama yake azikwa na mamia Babati Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mtoto aliouawa kwa kipigo cha mama yake azikwa na mamia Babati mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/mtoto-aliouawa-kwa-kipigo-cha-mama-yake.html
0 Response to "Mtoto aliouawa kwa kipigo cha mama yake azikwa na mamia Babati"
Post a Comment