Loading...
title : MWANAFUNZI UDOM AKWAMA NAULI, AOMBA MSAADA WA KUMPELEKA CHUONI
link : MWANAFUNZI UDOM AKWAMA NAULI, AOMBA MSAADA WA KUMPELEKA CHUONI
MWANAFUNZI UDOM AKWAMA NAULI, AOMBA MSAADA WA KUMPELEKA CHUONI
Na Yeremias Ngerangera, Namtumbo
Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa chuo kikuu cha Dodoma ( UDOM)kitivo cha elimu amekwama nauli ya kufika chuoni baada ya wazazi wake kutamka bayana kuwa hawana uwezo hata ya kupata nauli ya kumsafirisha binti yao kufika chuoni .
Bahati Njete (21) mkazi wa Minazini wilayani Namtumbo amechaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Dodoma huku wazazi wake hawana uwezo hata wa kumpatia nauli ya kufika chuoni ili akaendelee na masoma yake.
Akiongea na Ofisa ustawi wa jamii wilaya ya Namtumbo Irene Kitula ofisini kwake Bahati alisema wazazi wake wanahali ngumu za kimaisha na mafanikio aliyoyapata ni kutokana na misaada ya wasamaria wema ambao walijitolea kwa hali na mali kumsaidia toka kidato cha kwanza hadi cha sita.
Aidha Bahati alidai kumaliza elimu ya sekondari katika sekondari ya kata Narwi iliyopo wilayani Namtumbo na kisha kuchaguliwa kuendelea na masomo kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Igowole iliyopo mkoa wa Njombe.
Ofisa ustawi wa jamii alimfikisha mwanafunzi huyo mpaka ofisi ya mkuu wa wilaya ya Namtumbo ili apatiwe kibali cha kuomba kuchangiwa fedha kutoka kwa wasamaria wema ili aweze kufika chuoni na zimsaidie akiwa chuoni pia.
Kwa mujibu wa mwanafunzi mwenyewe Bahati alidai kusoma katika mazingira magumu kulingana na hali ngumu za wazazi wake lakini anawashukuru wasamaria wema walioweza kumchangia kwa hali na mali mpaka kufikia hapo alipofikia .
Hata hivyo anaendelea kuwaomba wasamaria wema hao wasichoke kumsaidia bali waendelee kumsaidia kupitia namba yake ya simu 0718792037 ili aweze kutimiza ndoto zake za maisha baada ya kumaliza chuo.
Hivyo makala MWANAFUNZI UDOM AKWAMA NAULI, AOMBA MSAADA WA KUMPELEKA CHUONI
yaani makala yote MWANAFUNZI UDOM AKWAMA NAULI, AOMBA MSAADA WA KUMPELEKA CHUONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWANAFUNZI UDOM AKWAMA NAULI, AOMBA MSAADA WA KUMPELEKA CHUONI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/mwanafunzi-udom-akwama-nauli-aomba.html
0 Response to "MWANAFUNZI UDOM AKWAMA NAULI, AOMBA MSAADA WA KUMPELEKA CHUONI"
Post a Comment