Loading...
title : NI JUKUMU LA WAZAZI KUSIMAMIA MAADILI YA VIJANA
link : NI JUKUMU LA WAZAZI KUSIMAMIA MAADILI YA VIJANA
NI JUKUMU LA WAZAZI KUSIMAMIA MAADILI YA VIJANA
NA ELISA SHUNDA,KIBAHA.
KONGAMANO la Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Iimetoka na Azimio la Pamoja la Wazazi katika Jamii Husika Kuhakikisha Inasimamia Maadili ya Vijana kwa Kuwa Chanzo cha Mmomonyoko wa Maadili Unaanzia kwenye vitongoji na mitaa ambako familia zao ndipo zinapoishi.
Maadili ni Mjumuisho wa Tabia Watu Zinazokubalika Mahali Fulani au Katika Jamii Fulani au Jumuiya Fulani au Nchi, Mjumuisho wa Tabia za Watu Unatokana na Kujumuisha Tabiaza Mtu mmoja Mmoja Tabia Hizi Ndizo Zinatufikisha Kule Tunapokuthamini.
Akizungumza baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kibaha Mjini,Edwin Shunda,alisema kuwa kwa mjumuisho wa kongamano hilo lililoshirikisha wadau mbalimbali kutoka taasisi mbalimbali,wananchi na wanachama wa CCM imeazimia kwa pamoja kuwa mmomonyoko wa vijana katika maadili yao inatokana na malezi ya wazazi lakini pia katika mitaa na vitongoji ambavyo vijana hao wanatokea hakuna malezi ya pamoja ya wazazi kwa vijana wa sehemu husika kwa kuogopa lawama kwa wazazi wa motto au watoto waliovunja hayo maadili.
“Katika majadiliano yaliyofanyika leo katika kongamano hili la maadili wajumbe wengi na wadau mbalimbali wamesema sababu kubwa inayochangia kupolomoka kwa maadili kwa watoto wetu ni wazazi sisi kwa sisi wenyewe kuogopana kuwa huyu mtoto siyo wangu ukimuadhibu au kumkanya kwa kosa ulilomkuta nalo kwa hali ya sasa unaweza ukanunua ugomvi kwa familia ya mtoto aliyefanya kosa hivyo kupitia kongamano hili tumeazimia kwa pamoja tunapotoka hapa tunaanzisha mabaraza ya jamii yatakayoanzishwa kwenye vijiji na mitaa kwa ajili ya kusimamia malezi na maadili ya watoto wetu” Alisema Mwenyekiti Shunda.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Kibaha Mjini,Edwin Shunda (katikati) akizungumza katika Kongamano la Maadili lililokuwa likijadili mmomonyoko wa maadili ya vijana yaliyofanyika katika ukumbi wa Shirika la Elimu Kibaha jana. Kulia ni Mjumbe wa Baraza hilo,Mwalimu Charles Maguye na Katibu wa Jumuiya Hiyo,Ruth Rutashiba. Picha na Elisa Shunda

Wajumbe na wanachama wa Chama Hicho wakifuatilia kwa umakini kongamano hilo.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>
Hivyo makala NI JUKUMU LA WAZAZI KUSIMAMIA MAADILI YA VIJANA
yaani makala yote NI JUKUMU LA WAZAZI KUSIMAMIA MAADILI YA VIJANA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NI JUKUMU LA WAZAZI KUSIMAMIA MAADILI YA VIJANA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/ni-jukumu-la-wazazi-kusimamia-maadili.html
0 Response to "NI JUKUMU LA WAZAZI KUSIMAMIA MAADILI YA VIJANA"
Post a Comment