Loading...
title : Serikali Kuendelea Kufutia Milki Mashamba Yaliyotelekezwa
link : Serikali Kuendelea Kufutia Milki Mashamba Yaliyotelekezwa
Serikali Kuendelea Kufutia Milki Mashamba Yaliyotelekezwa
Na: Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma.
Serikali imeendelea kuchukua hatua za kubatilisha milki za ardhi za mashamba yaliyotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Hayo yamesema Bungeni leo na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angelina Mabula wakati akijibu swali la Mhe. Dustan Kitandula Mbunge wa Mkinga kuhusu kufuta hati za mashamba yaliyotelekezwa.
"Katika kipindi cha Disemba, 2015 mpaka Octoba, 2018 mashamba yenye ukubwa wa ekari 84,240.803 yamebatilishwa katika Halmashauri za Ngorongoro, Arumeru, Moshi, Kinondoni,(Manispaa), Kigamboni(Manispaa), Mvomero, Kilombero, Kilosa, Mvomero, Iringa, Bukoba, Tarime, Kibaha, Serengeti, Busega, Muheza, Lushoto na Mkinga" amefafanua Naibu Waziri Mabula.
Mabula anasema kuwa, katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Shamba Na. 278 Mkomazi lenye ukubwa wa ekari 15,442 lililokuwa likimilikiwa na kampuni ya M/S Mkomazi Plantations Limited kwa Hati Namba 4268, 9780 na 9781 milki yake ilithibitishwa tarehe 20 Juni, 2018.
Aidha anafafanua kuwa, baada ya kubatilishwa kwa milki ya shamba hilo, Serikali ya Mkoa wa Tanga kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga zipange matumizi mapya ya shamba hilo kwa kuzingatia mahitaji ya ardhi katika eneo hilo kipaumbele kikiwa ni mahitaji ya wananchi na ardhi kwa ajili ya uwekezaji.
Mbali na hayo Mabula amezitaka Halmashauri zote nchini kubaini mashamba yaliyotelekezwa kutuma ilani kwa wamiliki wa mashamba hayo kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi (Sura 113) na kuwasilisha mapendekezo katika Wizara ya Ardhi kwa hatua za kubatilisha milki za mashamba hayo ziweze kufanyika.
Hivyo makala Serikali Kuendelea Kufutia Milki Mashamba Yaliyotelekezwa
yaani makala yote Serikali Kuendelea Kufutia Milki Mashamba Yaliyotelekezwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali Kuendelea Kufutia Milki Mashamba Yaliyotelekezwa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/serikali-kuendelea-kufutia-milki.html
0 Response to "Serikali Kuendelea Kufutia Milki Mashamba Yaliyotelekezwa"
Post a Comment