Loading...

SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA KIWANDA CHAI MPONDE

Loading...
SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA KIWANDA CHAI MPONDE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA KIWANDA CHAI MPONDE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA KIWANDA CHAI MPONDE
link : SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA KIWANDA CHAI MPONDE

soma pia


SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA KIWANDA CHAI MPONDE

*Yaagiza mashine zichunguzwe, mitambo yenye hitilafu ikarabatiwe kazi ianze
SERIKALI imemaliza mgogoro uliodumu kwa miaka mingi kati ya wakulima wa chai wa wilaya za Lushoto na Korogwe na kampuni ya Mponde Tea Estate uliosababisha kufungwa kwa kiwanda cha chai cha Mponde baada ya kuagiza kiwanda hicho kianze kazi.

“Waziri Mwijage na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilomo Prof. Siza Tumbo hakikisheni kazi ya kukagua kiwanda na mitambo inafanyika haraka na kubaini mitambo ipi ni mizima na ipi ina hitilafu ili ukarabati ufanyike na kiwanda kianze kazi mara moja.”

Uamuzi huo wa Serikali umetangazwa leo (Alhamisi, Novemba 1, 2018) na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kweminyasa kata ya Mponde, wilayani Lushoto baada ya kutembelea kiwanda hicho .

Waziri Mkuu amesema mwaka 1999 Serikali iliamua kuwapa wakulima wa chai na kiwanda hicho  kwa ajili kuwawezesha kuwa na sehemu ya kuchakata chai yao lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kiuchumi. Imeamua kukirudisha Serikali baada ya kuwepo migogoro iliyoathiri uzalishaji kiwandani hapo.

Kuhusu suala la madeni ya watumishi, ameagiza watafutwe na madai yaorodheshwe kwa ajili ya malipo, amewahakikisha wananchi hao kuwa suala la ajira ambazo zilipotea baada ya kiwanda kufungwa zitarudi kwa sababu Serikali inataka kuona kiwanda kikifanya kazi.

“Serikali imeamua kukichukua kiwanda hiki ambacho awali ilikikabidhi wakulima wa chai na kwamba itahakikisha lengo lake la kuboresh kilimo linafanikiwa na  wakulima wanaendelea kulima zao la chai. Hatutaki kusikia masuala ya Utega wala Mponde hapa si mahali pake.”
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto Novemba 1, 2018.  Kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mitambo ya kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Novemba 1, 2018. Alikuwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha Chai cha Mponde wilayani Lushoto, Novemba 1, 2018. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela na wanne kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Bumbuli wilayani Lushoto akiwa katika ziara ya Mkoa wa Tanga, Novemba 1, 2018. 
 Wananchi wakimpungia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipowasili kwenye kijiji cha Mponde wilayani Lushoto kukagua kiwanda cha chai cha Mponde na kuzungumza na wananchi, Novemba 1, 2018.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA KIWANDA CHAI MPONDE

yaani makala yote SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA KIWANDA CHAI MPONDE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA KIWANDA CHAI MPONDE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/serikali-yamaliza-mgogoro-wa-kiwanda.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YAMALIZA MGOGORO WA KIWANDA CHAI MPONDE"

Post a Comment

Loading...