Loading...
title : TFDA YATOA SOMO LA KUDHIBITI SUMUKUVU KWA WASINDIKAJI WA UNGA MCHANGANYIKO NA SIAGI YA KARANGA
link : TFDA YATOA SOMO LA KUDHIBITI SUMUKUVU KWA WASINDIKAJI WA UNGA MCHANGANYIKO NA SIAGI YA KARANGA
TFDA YATOA SOMO LA KUDHIBITI SUMUKUVU KWA WASINDIKAJI WA UNGA MCHANGANYIKO NA SIAGI YA KARANGA
Mgeni Rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo (aliyekaa katikati) akiwa na viongozi wengine, kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula kutoka TFDA Makao Makuu, Immaculata Justine (wa nne); Kaimu Meneja wa TFDA Kanda ya Kaskazini, Bw. Ben Mcheza (wa pili); Mwenyekiti wa mafunzo hayo Bw. Mathias Msemo (wa kwanza) na Katibu wa Mafunzo husika Bi. Agata Tuheri wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Serikali walioshiriki katika tukio hilo.
Mgeni Rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wasindikaji wa Manispaa ya Arusha.
Mgeni Rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wasindikaji wa Halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Arusha.
Mtaalam wa TFDA, Bw. Kaiza Kilango akiwasilisha mojawapo ya mada ya udhibiti wa sumu kuvu.
Na: James Ndege Arusha
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) inaendesha kampeni ya kuhamasisha wasindikaji wa unga mchanganyiko wa mahindi na nafaka nyingine maarufu kama unga wa lishe pia siagi ya karanga ili kudhibiti sumu kuvu.
“Sumukuvu (Aflatoxin) hutokana na aina ya ukungu (fangasi) unaoota zaidi kwenye mazao ya mahindi na karanga na huweza kutokea katika mazao haya wakati yakiwa shambani, kuvunwa , kusafirishwa au kuhifadhiwa endapo wahusika hawatazingatia ushauri wa wataalam. Kabla ya kusindika, ikitokea wasindikaji hawajachambua mazao hayo na kuondoa mabovu na kuyateketeza ili yasiliwe na binadamu au wanyama, bidhaa hizo zitakuwa na kiwango kikubwa cha sumukuvu na hivyo kuathiri afya ya watumiaji kwa kuwa atakayekula kiwango kidogo kidogo cha sumu hiyo anaweza kupata madhara baada ya muda mrefu kama vile saratani ya ini, upungufu wa kinga na udumavu.
Vile vile atakayekula kiasi kikubwa cha sumu hiyo kwa muda mfupi, huweza kupata madhara makubwa ya kiafya ya kuharibika ini hata kusabisha kifo, hivyo ni muhimu wasindikaji wetu mzingatie ushauri wa TFDA katika kusindika bidhaa zenu ili kulinda afya ya jamii lakini pia kupata masoko ya ndani na nje ya nchi” alisema Kaimu Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa TFDA Makao Makuu, Bi. Immaculata Justine wakati wa maelezo ya awali ya ufunguzi wa mafunzo ya Wajasiriamali wapatao 70 wa Mkoa wa Arusha.
Mgeni Rasmi katika mafunzo hayo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo katika hotuba yake ya ufunguzi alisema “Ubora na Usalama wa vyakula vinavyosindikwa na Wasindikaji nchini ni jambo la msingi kwa afya za Wananchi. Vyakula ni bidhaa muhimu na nyeti kwa usalama wa jamii na kamwe Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli haitakubali vyakula visivyo na ubora viingie katika soko la Tanzania”.
“Vyakula duni visivyo na ubora vikiingia katika mzunguko wa soko vitaleta madhara makubwa kwa afya za watumiaji lakini pia vitakosa soko la ndani na nje ya nchi hivyo kudumaza ukuaji wa sekta ya viwanda nchini. Mafunzo haya ya udhibiti wa sumu kuvu yatawasaidia wasindikaji wetu kuweza kuzalisha bidhaa za chakula salama na bora kwa mujibu wa vigezo vya kisheria”.
Mafunzo hayo yameshirikisha pia Watalam kutoka SIDO Makao Makuu, Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) Makao Makuu, Halmashauri na Mkoa katika Idara za Afya, Lishe, Kilimo na mifugo ili yaweze kuwa endelevu. Ndani ya wiki mbili sasa, mafunzo kama haya yamefanyika katika mikoa ya Dodoma na Morogoro na mikakati inaendelea katika maeneo yaliyosalia.
Hivyo makala TFDA YATOA SOMO LA KUDHIBITI SUMUKUVU KWA WASINDIKAJI WA UNGA MCHANGANYIKO NA SIAGI YA KARANGA
yaani makala yote TFDA YATOA SOMO LA KUDHIBITI SUMUKUVU KWA WASINDIKAJI WA UNGA MCHANGANYIKO NA SIAGI YA KARANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TFDA YATOA SOMO LA KUDHIBITI SUMUKUVU KWA WASINDIKAJI WA UNGA MCHANGANYIKO NA SIAGI YA KARANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/tfda-yatoa-somo-la-kudhibiti-sumukuvu.html
0 Response to "TFDA YATOA SOMO LA KUDHIBITI SUMUKUVU KWA WASINDIKAJI WA UNGA MCHANGANYIKO NA SIAGI YA KARANGA"
Post a Comment