Loading...
title : UJENZI WA DARAJA KATIKA ZIWA VICTORIA KUANZA MWAKANI
link : UJENZI WA DARAJA KATIKA ZIWA VICTORIA KUANZA MWAKANI
UJENZI WA DARAJA KATIKA ZIWA VICTORIA KUANZA MWAKANI
Naibu Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Elias John Kwandikwa amewataka wakazi wa mikoa ya Mwanza na Geita kuchangamkia fursa za kiuchumi na kijamii zitakazojitokeza wakati wa ujenzi wa daraja litakalounganisha eneo la Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza.
Amesema maandalizi kwaajili ya ujenzi wa daraja hilo la aina yake hapa nchini yako katika hatua ya usanifu wa kina hivyo ujenzi wake utaanza mara baada ya mkandarasi wake kutangazwa na linatarajiwa kuwa na urefu wa kilomita 3.2, litakapokamilika. “Hakikisheni mnatoa ushirikiano kwa mkandarasi ili kazi ya ujenzi iwe nyepesi na wale watakaopata fursa za ajira fanyeni kazi kwa weledi, bidii na nidhamu” amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.
Amesema Serikali inatumia fedha nyingi katika miradi ya maendeleo ya muda mrefu hivyo ni jukumu la wananchi kujiandaa na kubaini fursa za kiuchumi na kijamii na kuzitumia. Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Mwanza Mhandisi Marwa Rubirya amesema daraja hilo litakuwa na njia nne za kupitisha magari, njia ya waenda kwa miguu ambapo pia litakuwa na kina kitakachoruhusu meli kupita chini ya daraja hilo.
Mhandisi Rubirya amesisitiza umuhimu wa wananchi wenye maeneo yatakayotumika kupisha ujenzi huo kutoa ushirikiano ili kuharakisha kazi hiyo. Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa amekagua kivuko cha Kigongo-Busisi na kuagiza Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), kuhakikisha elimu inatolewa kwa wananchi kuhusu usalama na matumizi sahihi ya utumiaji wa vivuko.
Amezungumzia umuhimu wa TEMESA kuweka mifumo ya kielektoniki ili kuwezesha waendesha vivuko, wakusanya mapato na wasimamizi kuwa na mawasiliano ya pamoja na hivyo kuwezesha vivuko kuwa na abiria na mizigo inayokubalika wakati wote. Mkuu wa kivuko cha Kigongo –Busisi Mhandisi Abdala Atiki amesema kivuko hicho kwa sasa kinahudumiwa na Mv- Mwanza na Mv- Misungwi ambapo zaidi ya abiria elfu sita na mia tano huvushwa kwa siku.
Zaidi ya mikoa 12 nchini ina maeneo yenye mahitaji ya vivuko ambapo takriban vivuko 30 vinatoa huduma nchini kote.
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mwanza Mhandisi Marwa Rubirya (katikati), akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (kushoto) eneo litakapojengwa daraja jipya linalounganisha Kigongo-Busisi mkoani Mwanza, daraja hilo litakuwa na urefu wa KM 3.2 kulia ni mkuu wa kivuko cha kigongo-busisi mhandisi Abdala Atiki.
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Mwanza Mhandisi Marwa Rubirya (watatu kushoto), akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (wapili kushoto) eneo litakapojengwa daraja jipya linalounganisha Kigongo-Busisi mkoani Mwanza, daraja hilo litakuwa na urefu wa KM 3.2 (kulia) ni mkuu wa kivuko cha Kigongo-Busisi mhandisi Abdala Atiki.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Elias John Kwandikwa (mwenye miwani), akiwasikiliza wanafunzi ambao ni abiria wa kivuko cha Mv- Mwanza kinachotoa huduma kati ya Kigongo-Busisi mkoani Mwanza alipokagua shughuli za uendeshaji wa kivuko hicho.
Hivyo makala UJENZI WA DARAJA KATIKA ZIWA VICTORIA KUANZA MWAKANI
yaani makala yote UJENZI WA DARAJA KATIKA ZIWA VICTORIA KUANZA MWAKANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UJENZI WA DARAJA KATIKA ZIWA VICTORIA KUANZA MWAKANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/ujenzi-wa-daraja-katika-ziwa-victoria.html
0 Response to "UJENZI WA DARAJA KATIKA ZIWA VICTORIA KUANZA MWAKANI"
Post a Comment