Loading...

VODACOM YATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WASICHANA.

Loading...
VODACOM YATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WASICHANA. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa VODACOM YATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WASICHANA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : VODACOM YATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WASICHANA.
link : VODACOM YATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WASICHANA.

soma pia


VODACOM YATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WASICHANA.


Na Mwandishi Wetu, Lindi.
Vodacom Tanzania Foundation kwa kushrikianana T-MARC wameendesha  programu ya kuwaelimisha wanafunzi wa shule ya msingiTulieni iliyopo mkoani Lindi kuhusu usafi wa kimwili wakati wa hedhi pamoja na  elimu ya afya ya uzazi.

Katika programa hiyo zaidi ya wasichana I700 waliopevuka wamepatiwa taulo za hedhi.

Programu hiyo ni sehemu ya mradi endelevu uitwao “Hakuna wasichoweza” unaofanyakazi na Vodacom Tanzania Foundation wakishirikianana T-MARC tangu mwaka 2012

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacquiline Materu alisema “Vodacom Foundation imejikita katika mipango ambayo inasaidia akina mama na watoto nchini, ili kuboresha afya zao, elimu, na ujasiriamali.
 Tunaipongeza sana serikali kwa kufuta kodi za sodo. 

"Sisi kama Vodacom Foundation tutaendelea kusaidia shughuli zozote ambazo zinalenga kutatua changamoto zinazowafanya wasichana washindwe kupata elimu bora”.

Alisema kuwa hakuna wasichoweza, kwani lengo ni kuboresha mahudhurio na ufaulu wa wasichana kwa kuwapatia elimu juu ya afya ya uzazi, elimu ya hedhi, jinsia,vile vile umuhimu wa kuchelewa kuanza kujihusisha na ngono.

Kwa miaka sita mpango huu umefikia wasichana zaidi ya elfu moja na zaidi ya taulo za kike 10,000 ziligawiwa.

“Kupitia msaada wa Vodacom Foundation, tumeona maendeleo katika mahudhurio na ufaulu wa wasichana ambao walihudhuria mafunzo haya ukilinganisha na ambao hawajahudhuria.

Alisema kuwa  vinavyowafanya wasichana waliopevuka kushindwa kufikia malengo yao ya kielimu kwa sababu ya changamoto mbalimbali wakati wa hedhi pamoja na afya ya uzazi kupitia vipindi vya mafunzo.

Hata hivyo ripoti iliyotolewana TASAWANET mwaka 2015 inaonyesha kwamba asilimia 75 ya wasichana mashuleni wamesema kwamba hedhi inaathiri kufaulu kwao katika masomo.

UNESCO imekadiria kwamba ndani ya mwaka mmoja, asilimia 20 ya wanafunzi wa kike hawahudhurii mashuleni.

Wsichana awawana nafasi ya kufikia malengo yao na tumedhamiria kuwafikia wasichana wengi zaidi hasa hasa katika miji iliyojificha na yenye mila na fikra potofu juu ya hedhi zinazochochea changamoto hizi” alisemaHamid Al-Alawy Mratibu wa Mradi, T-MARC Tanzania.



Hivyo makala VODACOM YATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WASICHANA.

yaani makala yote VODACOM YATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WASICHANA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala VODACOM YATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WASICHANA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/vodacom-yatoa-elimu-ya-afya-ya-uzazi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "VODACOM YATOA ELIMU YA AFYA YA UZAZI KWA WASICHANA."

Post a Comment

Loading...