Loading...

WAGANGA WA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA WATAKIWA KUFATA MAADILI YA KAZI.

Loading...
WAGANGA WA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA WATAKIWA KUFATA MAADILI YA KAZI. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAGANGA WA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA WATAKIWA KUFATA MAADILI YA KAZI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAGANGA WA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA WATAKIWA KUFATA MAADILI YA KAZI.
link : WAGANGA WA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA WATAKIWA KUFATA MAADILI YA KAZI.

soma pia


WAGANGA WA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA WATAKIWA KUFATA MAADILI YA KAZI.




Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Waganga wa tiba asili na tiba mbadala wametakiwa kufata maadili wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo kuto kuwadanganya wateja kuhusu kupata mali au utajiri.

Akizumguma leo jijini Dar es Salaam Msajili wa Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala nchini Dkt. Ruth Suza wakati wa semina na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa tiba  asili na tiba mbadala nchini.

Dkt. Suza amesema kuwa ni busara kila mganga wa tiba asili na tiba mbadala wakafata kanuni na utaratibu katika kutekeleza majukumu yao.

Hata hivyo amesema kuwa kuna waganga wa tiba asili na tiba mbadala 19912 wamesajiliwa na Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala nchini ili kuweza kutoa huduma hizo kwa kufuata sheria na taratibu.

 “Pamoja na waganga wa tiba asili na tiba mbadala 19912 kusajiliwa pia tumesajili vituo vya tiba asili na tiba mbadala 19  kutoa huduma za afya nchini” alisema Dkt. Suza.

Aidha Dkt. Suza amewataka waganga wa tiba asili na tiba mbadala kupitisha dawa zao kwenye mamlaka husika kwa ajili ya vipimo pamoja na kusajiliwa kwa matumizi sahihi ya watanzania.

Mbali na hayo Dkt. Suza amesema kuwa wakunga  wa jadi nchini wanatakiwa kuwa kipaumbele katika kuhakikisha wamama wajawazito wanawahimiza wamama wajawazito wanajifungulia katika vituo vya afya kwa usalama wa maisha ya mama na mtoto.

“Tunapita kuwaelimisha Wakunga wa jadi kuwa kazi yao kubwa ni kuhakikisha mama mjamzito anajifungua salama kwenye kituo cha afya kilichopo karibu ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi” alisema Dkt. Suza.


Kwa upande wake Mratibu wa Taifa wa masuala ya Tiba asili na tiba mbadala Dkt. Liggyle Vumilia amesema kuwa watanzania wanatakiwa kujitokeza kwenye kilimo cha uzalishaji wa miti ya dawa za asili na mbadala ili kupiga hatua zaidi kwenye huduma hizo nchini.

Naye Mfamasia kutoka Baraza la Tiba asili na Tiba mbadala Bw. Ndahani Msigwa amesema kuwa waganga hawatakiwi kutoa matangazo ya dawa zao ambazo hazijasajiliwa pamoja na kujitangaza kama hawajasajiliwa.

“Mganga wa tiba asili na tiba mbadala hatakiwi kutangaza dawa yake km hajasajili dawa hiyo na asijitangaze kama hana kibali maalum kutoka baraza hili iwe kwenye luninga, radio, magazeti hata mitandao ya kijamii”, alisema Bw. Msigwa.

Aidha Bw. Ndahani amesema kuwa waganga hawatakiwi kukata vimeo kwa watoto, kukeketa, kutoa meno ya plastiki pamoja na kupiga ramli kwani ni kinyume cha sheria na taratibu za baraza hilo.

Bw. Ndahani amesema kuwa waganga wanatakiwa kuzingatia usiri pindi wanapowahudumia wateja wao na kuweka mazingira ya kutolea huduma zao kuwa na usafi pamoja na usalama wa wateja.


Hivyo makala WAGANGA WA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA WATAKIWA KUFATA MAADILI YA KAZI.

yaani makala yote WAGANGA WA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA WATAKIWA KUFATA MAADILI YA KAZI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAGANGA WA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA WATAKIWA KUFATA MAADILI YA KAZI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/waganga-wa-tiba-asili-na-tiba-mbadala.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAGANGA WA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA WATAKIWA KUFATA MAADILI YA KAZI."

Post a Comment

Loading...