Loading...
title : Watoto wa kike Manispaa ya Ilala watakiwa kujengewa misingi bora
link : Watoto wa kike Manispaa ya Ilala watakiwa kujengewa misingi bora
Watoto wa kike Manispaa ya Ilala watakiwa kujengewa misingi bora
Na Heri Shaaban
Mwambawahabari
Wazazi na Walezi wa Manispaa ya Ilala watakiwa kujengea watoto wa kike misingi bora katika malezi yao na kufuata maadili mema ili wasinginze katika tabia ya vitendo hatarishi.
Hayo yalisemwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Sophia Ntomola wakati wa siku ya madhimisho ya Mtoto wa kike Kata ya Buguruni.
Ntomola alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wa kike kutokana na maumbile yao,na mila na desturi zilizojengeka miongoni mwa wana jamii kwamba mtoto wa kike sio muhimu katika familia na jamii.
"Wazazi na walezi ndani ya manispaa ya Ilala mnawajibu mkubwa kuwajengea misingi bora watoto wa kike na kuwapatia elimu kwa manufaa ya Taifa "alisema Ntomola
Ntomola alisema utandawazi ,elimu duni miongoni mwa wazazi ,walezi wamekuwa wakisababisha kutokupewa nafasi ya kusikilizwa matatizo yao na kujifunza mambo tofauti na utamaduni wetu,kupelekea vijana kujiingiza katika tabia hatarishi ambazo zinaathari kiafya kupelekea kushindwa kutimiza ndoto zao.
Alisema tabia hizo za vitendo hatarishi vinasababisha watoto wengi wa kike kushindwa kutimiza ndoto zao.
Aidha alisema miongoni mwa tabia hizo zinapelekea kupata mimba za utotoni ,mimba zisizo tarajiwa,magonjwa yatokanayo kujamiana ikiwemo UKIMWI pamoja ongezeko la vifo vinavyotokana na uzazi.
Ntomola alisema Tanzania miongoni mwa nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ambazo zinazoathirika zaidi na watoto wa kike kushindwa kufikia ndoto zao kutokana na sababu mbalimbali.
Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii kata ya Buguruni Rose Chundu alisema ukatili dhidi ya watoto wa kike ni tatizo kubwa katika jamii linathiri afya ya jamii na upatikanaji wa haki za Binadamu nchini Tanzania.
Rose alisema katika kata ya Buguruni Mwezi Julai hadi Octobar wamepokea kesi 69 walalamikaji wote wanawake hii inaonyesha kuwa wanawake ndio wanabeba jukumu kubwa la kutunza watoto hivyo alishauri watoto wa kike wajengewe uwezo tangu wakiwa wadogo ili waweze kujitegemea.
Alitaka jamii ihakikishe mtoto wa kike anawezeshwa kielimu ,ili apate stadi mbalimbali za kujitegemea na kuakikisha wanapata malezi chanya ili kuleta ukaribu kati ya wazazi ,walezi .
Hivyo makala Watoto wa kike Manispaa ya Ilala watakiwa kujengewa misingi bora
yaani makala yote Watoto wa kike Manispaa ya Ilala watakiwa kujengewa misingi bora Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Watoto wa kike Manispaa ya Ilala watakiwa kujengewa misingi bora mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/watoto-wa-kike-manispaa-ya-ilala.html
0 Response to "Watoto wa kike Manispaa ya Ilala watakiwa kujengewa misingi bora"
Post a Comment