Loading...

WAZIRI KAIRUKI AAGIZA RITA KUVUNJA BODI YA UONGOZI WA MFUKO WA UDHAMINI WA NORTH MARA

Loading...
WAZIRI KAIRUKI AAGIZA RITA KUVUNJA BODI YA UONGOZI WA MFUKO WA UDHAMINI WA NORTH MARA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI KAIRUKI AAGIZA RITA KUVUNJA BODI YA UONGOZI WA MFUKO WA UDHAMINI WA NORTH MARA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI KAIRUKI AAGIZA RITA KUVUNJA BODI YA UONGOZI WA MFUKO WA UDHAMINI WA NORTH MARA
link : WAZIRI KAIRUKI AAGIZA RITA KUVUNJA BODI YA UONGOZI WA MFUKO WA UDHAMINI WA NORTH MARA

soma pia


WAZIRI KAIRUKI AAGIZA RITA KUVUNJA BODI YA UONGOZI WA MFUKO WA UDHAMINI WA NORTH MARA

Na Asteria Muhozya, Mara
Waziri wa Madini Angellah Kairuki ameuagiza Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kuvunja uongozi wa Mfuko wa Udhamini wa North Mara ( Bodi ya Wadhamini na Menejimenti) kwa kuwa umeshindwa  kusimamia  uendeshaji wa Mfuko kwa tija na kuandaa utaratibu mzuri  wa usimamizi  wa Mfuko huo ambao utakuwa na  manufaa kwa Taifa .

Aidha, Waziri Kairuki amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Tarime kuruhusu fedha za Keng'anya Enterprises Ltd ( KEL) kuendelea kulipwa  hadi hapo vyombo vya uchunguzi vitakakapobaini na kuelekeza vinginevyo, huku Mkuu wa Mkoa wa Mara akitakiwa kusimamia utekelezaji wa agizo hilo.

“Kwa kuwa Keng'anya Enterprises iliomba kupata PL 303/95 kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia Sekta ya Madini, hivyo malipo ya mrabaha wa asilimia moja yanayopokelewa kutoka kwenye mgodi kwa mujibu wa mkataba wake ni halali,” alisisitiza Kairuki.

Waziri Kairuki  alitoa  maagizo hayo Novemba 21, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ambaye alielekeza kufanyika uchunguzi wa Mfuko wa North Mara Community Trust  Fund, baada  ya baadhi ya wananchi wa Nyamongo Wilayani  Tarime kulalamika juu ya jamii kutofaidika na mfuko huo na badala yake kunufaisha baadhi ya watu wachache.

Rais Magufuli alitoa maelekezo ya kufanyika kwa uchunguzi wa mfuko huo wakati wa ziara yake Mkoani Mara tarehe 4 hadi 8 Septemba, 2018.

Mbali na agizo la kuuvunja uongozi wa mfuko, Waziri Kairuki aliiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuwachunguza na kuwachukulia hatua za kisheria wajumbe wa bodi ya wadhamini, menejimenti ya mfuko na yeyote atakayethbitika kujihusisha na ufujaji na matumizi mabaya ya fedha za mfuko.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akieleza jambo. Kulia ni Mkuu wa MKoa wa Mara, Adam Malima na kushoto ni Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko
Waziri wa Madini Angellah Kairuki akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kulia)
Sehemu ya Watendaji kutoka Wizara ya Madini, Uongozi wa Mkoa  wa Mara wakifuatilia kikao hicho.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WAZIRI KAIRUKI AAGIZA RITA KUVUNJA BODI YA UONGOZI WA MFUKO WA UDHAMINI WA NORTH MARA

yaani makala yote WAZIRI KAIRUKI AAGIZA RITA KUVUNJA BODI YA UONGOZI WA MFUKO WA UDHAMINI WA NORTH MARA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KAIRUKI AAGIZA RITA KUVUNJA BODI YA UONGOZI WA MFUKO WA UDHAMINI WA NORTH MARA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/waziri-kairuki-aagiza-rita-kuvunja-bodi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI KAIRUKI AAGIZA RITA KUVUNJA BODI YA UONGOZI WA MFUKO WA UDHAMINI WA NORTH MARA"

Post a Comment

Loading...