Loading...

WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE

Loading...
WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE
link : WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE

soma pia


WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE



*Aagiza wakurugenzi wakuu wa NSSF, AZIMIO, Kamishna TRA wakutane.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa nyumba unaojengwa kwa ubia kati Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kampuni ya Azimio Housing Estate Limited katika eneo la Dege Beach Kigamboni na kutamka kuwa amesikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaendelea kwenye eneo hilo.

Amewaagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio na Mkurugenzi wa Mkuu kampuni ya Azimio Housing Estate Limited, Mohammed Iqbal wakutane na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere ili wajadiliane namna ya kudhibiti wizi na kuimarisha ulinzi. 

Waziri Mkuu alitembelea eneo la mradi huo jana jioni (Jumatatu, Novemba 12, 2018) ambapo baada ya kufika katika eneo ambalo linajengwa nyumba zaidi ya 7,000 alionesha kusikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaoendelea na kutoa maagizo kwa wahusika.

“Kuna mpango gani wa ulinzi wa mali hapa, mali zinaendelea kuibiwa, tutakuja kuanza ujenzi hapa na kukuta hakuna mali hata moja. Ulinzi lazima uimarishwe pande zote mbili za mradi huu eneo la ujenzi na eneo la kuhifadhia vifaa vya ujenzi.”
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia Majengo ya  DEGE ECO- VILLAGE  mradi wa   ubia kati ya Shirika la hifadhi ya Jamii NSSF na Azimiao wa Nyumba 7,4460 zilizopo  Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam .jana  Novemba 12/2018 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa . katikati mwenye Tai nyekundu   atembelea DEGE ECO- VILLAGE  mradi wa   ubia kati ya Shirika la hifadhi ya Jamii NSSF na Azimio wa Nyumba 7,4460 zilizopo  Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam .kulia  ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF .Wiliam Erio na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Azimio. Mohammed Iqbal. Waziri Mkuu ametembelea mradi huo jana  Novemba 12/2018.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa . katikati mwenye Tai nyekundu   atembelea DEGE ECO- VILLAGE  mradi wa   ubia kati ya Shirika la hifadhi ya Jamii NSSF na Azimiao wa Nyumba 7,4460 zilizopo  Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam .kulia  ni Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF Balozi Ali Siwa.na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Azimiao. Mohammed Iqbal. Waziri Mkuu ametembelea mradi huo jana  Novemba 12/2018.



Hivyo makala WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE

yaani makala yote WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/waziri-mkuu-asikitishwa-wizi-kwenye.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI MKUU ASIKITISHWA WIZI KWENYE MRADI WA NSSF DEGE"

Post a Comment

Loading...