Loading...
title : Waziri wa Maliasi na Utalii Dkt.Kigwangalla Aitega Bodi ya Wadhamini ya TaFF
link : Waziri wa Maliasi na Utalii Dkt.Kigwangalla Aitega Bodi ya Wadhamini ya TaFF
Waziri wa Maliasi na Utalii Dkt.Kigwangalla Aitega Bodi ya Wadhamini ya TaFF
Na Lusungu Helela-Dodoma
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameiagiza Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF) isimamie utekelezaji wa uanzishwaji wa mradi wa viwanda vya kusindika, kuchakata na kufungasha asali katika mikoa inayofuga nyuki ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo na kujenga uchumi wa viwanda
Waziri Kigwangalla ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizindua Bodi ya pili ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania uliofanyika leo jijini Dodoma.
Kufuatia agizo hilo, Waziri Kigwangalla ameiambia Bodi hiyo kuwa pamoja na utekelezaji wa maagizo mengine aliyowapatia, suala la uanzishwaji viwanda vya kusindika, kuchakata na kufungasha asali na bidhaa nyingine zitokanazo na ufugaji nyuki katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe na Mbeya liinapaswa kupewa uzito wa juu kiutekelezaji.
Waziri Kigwangala ameongeza kuwa ni azma ya Serikali ya awamu ya tano kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati ifikapo 2025 na kuwa suala hilo lina umuhimu mkubwa kwa wafugaji wa nyuki na uhifadhi mazingira..
Ameongeza kuwa endapo suala hilo la viwanda litafanikiwa , itasaida kuchochea jamii kuwa mstari wa mbele kulinda misitu badala ya sasa jamii kujikita kwenye ukataji miti ovyo hali inayotishia nchi kugeuka kuwa jangwa kama hatua za haraka hazitachukuliwa.
Amesema kiwango cha ufugaji nyuki kwa mikoa inayofuga si cha kuridhisha kwa vile wafugaji walio wengi wamekuwa wakifuga kwa mazoea jambo ambalo wafugaji walio wengi kuamua kuachana na shughuli hiyo na kugeukia uchomaji mkaa pamoja na kujiingiza kwenye shughuli za uharibifu mazingira.
Waziri Kigwangalla amesema uanzishwaji wa viwanda hivyo vitasaidia jamii kuwa na kipato mbadala hali itakayopelekea wananchi kuanza kuona umuhimu wa kulinda na kuhifadhi misitu.
"Mkianza kuwekeza upande wa magharibi ambapo kuna zaidi ya asilimia 60 ya misitu yote hapa nchini wananchi, wakiwemo Nzega, Sikonge, Uyui, Tanganyika, Mlele, Mpanda na Kaliua hawatakubali kuona mtu au kikundi cha watu kinaharibu misitu.
"Nataka kuona mapinduzi makubwa kwenye ufugaji nyuki kwa kuiwezesha jamii kuwa na mizinga ya kisasa ili iweze kufuga nyuki kisasa na hatimaye wapeleke kwenye viwanda wakajifunze kufungasha kisasa, ili ipate bei kubwa, na mwisho wa siku wataona faida ya kuwa na misitu.
Wakati huo huo, Waziri Kigwangalla ameitaka Bodi hiyo isimamie utekelezaji wa uhuishaji wa misitu ya kijiji pamoja na ile ya Halmashauri ambayo tayari imeharibiwa kwa kuanza kupanda miti ya asili pamoja na kuanzisha mashamba mapya ya miti.
Naye, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe, Constantine Kanyasu ameitaka Bodi hiyo isimamie utekelezaji wa upandaji miti kwa vile mikoa kama Shinyanga hali ya uharibifu misitu inatisha,
Ameongeza kuwa kama hatua za makusudi hazitachukuliwa itafika kipidi ambacho akina mama wa vijijjini watakuwa wakitembea umbali wa kilomita 200 kwa ajili yua kutafuta kuni
Awali, Kaimu Katibu ,Mkuu wa Wizara hiyo, Lucius Mwenda amesema tangu kuanzishwa kwa Mfuko huo umekuwa ukisaidia sana kwenye uhifadhi licha ya kuwa mfuko huo umekuwa na changamoto ya uhaba wa watumishi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof. Romanus Ishengoma amemhakikishia Waziri Kigwangalla kuwa Wajumbe wa Bodi watafanya kazi kwa weledi na utaalamu wa hali ya juu na kuanza na suala la uanzishwaji wa viwanda vitavyowasaidia wafugaji nyuki nchini.
Hivyo makala Waziri wa Maliasi na Utalii Dkt.Kigwangalla Aitega Bodi ya Wadhamini ya TaFF
yaani makala yote Waziri wa Maliasi na Utalii Dkt.Kigwangalla Aitega Bodi ya Wadhamini ya TaFF Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri wa Maliasi na Utalii Dkt.Kigwangalla Aitega Bodi ya Wadhamini ya TaFF mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/waziri-wa-maliasi-na-utalii.html
0 Response to "Waziri wa Maliasi na Utalii Dkt.Kigwangalla Aitega Bodi ya Wadhamini ya TaFF"
Post a Comment