Loading...
title : Atakaegundulika kuhusika na kuvuja kwa mitihani ya kidato cha pili kukiona: Waziri
link : Atakaegundulika kuhusika na kuvuja kwa mitihani ya kidato cha pili kukiona: Waziri
Atakaegundulika kuhusika na kuvuja kwa mitihani ya kidato cha pili kukiona: Waziri
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma akizungumza na Kamati ya Baraza la Mitihani Zanzibar kuhusu hatua zitazochukuliwa baada ya kufutwa Mtihani wa Kidatu cha pili mwaka 2018 katika Kituo cha Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Unguja.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mmanga Mjengo Mjawiri akionyesha kuchukizwa na kitendo cha kuvujisha Mtihani wa Kidatu cha Pili mwaka 2018 katika mkutano na Kamati ya Baraza la Mitihani uliofanyika Ukumbi wa Kituo cha Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Unguja.
Baadhi ya Watendaji wa Baraza la Mitihani Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma (hayupo pichani) alipokutana nao katika Kituo cha Elimu Mbadala Rahaleo kufuatia kuvuja Mtihani wa Kidatu cha Pili mwaka 2018
Picha na Maryam Kidiko – Maelezo Zanzibar.
Na Mwashungi Tahir Maelezo
Waziri wa Elimu mafunzo na amali Riziki Juma Pembe alisema Wizara haitomuonea haya kwa yeyote atakaegundulika kuhusika iwe kuchangia au kusababisha mitihani kuvuja sheria itachukua mkondo wake hata awe mtu wa karibu.
Hayo ameyasema huko katika ukumbi wa Mbadala Rahaleo wakati alipokuwa akizungumza na watendaji wa Baraza la mitihani kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuhusu kuvuja kwa mitihani na kukiri kuwa mitihani mengine itafanywa hapo tarehe itapotangazwa .
Aidha alisema tumeakhirisha kwa sababu tungeendelea nayo tungefanya maamuzi siyo ya haki kwa walokuwa hawakupata tusingeliwatendea haki.
Alisema iwapo atagundulika mtu yeyote hata awe na ukaribu wa aina gani gani Wizara haitoweza kumvumilia hatua za sheria za utumishi zitachukuliwa ili iwe fundisho kwa wengine na tukio hili lisiweze kutokea tena.
Aliwaomba watendaji wote kuwa na ushirikiano ili ziondoke athari zilizojitokeza , pia suala la uzembe kama hili lisitokee tena watendaji wajiamini kwani walijikubalisha na walikula kiapo hivyo waache tamaa na wawe waadilifu hata Mwenyezi Mungu anahimiza uadilifu.
“Naomba mashirikiano katika utendaji mzima wa kazi ili uzembe huu usitokee tena kwani kila mtu alikula kiapo katika utendaji wake wa kazi muhali uondoke tutakwenda sambamba na nitakula nae sahani moja ”.Alisema Waziri huyo.
Nae Naibu Waziri Mmanga Mjengo Mjawiri alisema kiongozi yeyote aliyelelewa vizuri hakubali kwenda kinyume na kazi yake lazima atakuwa yuko makini na utendaji kazi zake.
Alisema hili ni tukio la aibu limetokea na hivyo tuwe makini suala hili lisijirejee tena kwani lineondosha uaminifu kwa jamii na hasara kwa Serikali , wanafunzi na walimu pamoja na wazee.
Hivyo makala Atakaegundulika kuhusika na kuvuja kwa mitihani ya kidato cha pili kukiona: Waziri
yaani makala yote Atakaegundulika kuhusika na kuvuja kwa mitihani ya kidato cha pili kukiona: Waziri Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Atakaegundulika kuhusika na kuvuja kwa mitihani ya kidato cha pili kukiona: Waziri mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/atakaegundulika-kuhusika-na-kuvuja-kwa.html
0 Response to "Atakaegundulika kuhusika na kuvuja kwa mitihani ya kidato cha pili kukiona: Waziri"
Post a Comment