Loading...

BALOZI WA NORWAY NCHINI AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI

Loading...
BALOZI WA NORWAY NCHINI AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa BALOZI WA NORWAY NCHINI AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : BALOZI WA NORWAY NCHINI AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI
link : BALOZI WA NORWAY NCHINI AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI

soma pia


BALOZI WA NORWAY NCHINI AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI

Na Veronica Simba - Dodoma
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen leo Desemba 10, amemtembelea Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma na kufanya mazungumzo kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya nishati nchini.

Balozi Jacobsen amemweleza Naibu Waziri kuwa kampuni mbalimbali nchini mwake zina nia ya kuwekeza katika sekta ya nishati nchini na baadhi yake ziko katika hatua nzuri kwani tayari zimewasilisha serikalini mchanganuo wake unaoainisha sifa walizonazo wakisubiri zoezi la kushindanishwa na kampuni nyingine ili kupata zabuni husika za uwekezaji.

“Mojawapo ya kampuni hizo ina nia ya kuwekeza katika uzalishaji wa umeme wa upepo eneo la Makambako, ambapo ni ubia baina yake (52%) na wazawa (48%),” amesema Balozi. Kwa upande wake, Naibu Waziri Mgalu amemshukuru Balozi Jacobsen ambaye ni mwakilishi wa Serikali ya Norway kutokana na ushirikiano ambao nchi hiyo imekuwa ikiuonesha kwa Tanzania ikiwemo uwekezaji nchini na pia kufadhili wanafunzi katika masomo ya fani za gesi na mafuta.

Aidha, amemweleza Balozi huyo kuwa bado zipo fursa nyingi za uwekezaji katika sekta ya nishati nchini na hivyo ametumia fursa hiyo kuendelea kukaribisha kampuni mbalimbali za Norway kuja kuwekeza.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akifafanua jambo kwa Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen wakati Balozi huyo alipomtembelea mapema leo, Desemba 10, 2018 ofisini kwake Dodoma, kujadili fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen baada ya mazungumzo yao kujadili fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati mapema leo, Desemba 10, 2018 Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kushoto) akiagana na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Elisabeth Jacobsen, baada ya mazungumzo yao kujadili fursa za uwekezaji katika sekta ya nishati mapema leo, Desemba 10, 2018 Makao Makuu ya Wizara jijini Dodoma.


Hivyo makala BALOZI WA NORWAY NCHINI AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI

yaani makala yote BALOZI WA NORWAY NCHINI AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI WA NORWAY NCHINI AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/balozi-wa-norway-nchini-afanya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "BALOZI WA NORWAY NCHINI AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA NISHATI"

Post a Comment

Loading...