Loading...
title : BASATA YAWAONYA DIAMOND NA RAYVAN, HATUA KALI KUCHUKULIWA DHIDI YAO
link : BASATA YAWAONYA DIAMOND NA RAYVAN, HATUA KALI KUCHUKULIWA DHIDI YAO
BASATA YAWAONYA DIAMOND NA RAYVAN, HATUA KALI KUCHUKULIWA DHIDI YAO
*Ni baada ya kusambaza taarifa ya kuruhusiwa kufanya maonesho nje ya nchi.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaonya wasanii kutoka kundi la WCB Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz 'na Msanii mwenzake Raymond Mwakyusa 'Rayvan' kuacha kusambaza taarifa za uongo.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa BASATA Onesmo Kayanda baada ya wasanii hao kutoa kauli jana ya kuruhusiwa kufanya maonesho nje ya nchi baada ya kuwaandikia barua baraza na kuwaomba na wakawaruhusu.
Baraza limekanusha habari zinazosambaa kwenye vyombo vya habari hususani mitandao ya kijamii kuwa limewaruhusu Diamond na Rayvan.
Mnamo Desemba 18 2018, Baraza liliwafungia wasanii hao kutokujiahughulisha na sanaa ndani na nje ya nchi kwa kipindi kisichojulikana kutokana na kutumia kwa makusudi wimbo wa Mwanza ambao umefungiwa kwa sababu za kimaadili.
Baraza limeendelea kusisitiza kuwa halijawafungulia wasanii hao Diamond na Rayvan kufanya onesho lolote la sanaa ndani na nje ya nchi.
Aidha, baraza kwa mara nyingine linawataka wasaii hao kutii maagizo waliyopewa na kuacha mara moja kupotosha umma kwa kusambaza taarifa za uongo kabla ya hatua kali zaidi kuchukuliwa dhidi yao.
Hivyo makala BASATA YAWAONYA DIAMOND NA RAYVAN, HATUA KALI KUCHUKULIWA DHIDI YAO
yaani makala yote BASATA YAWAONYA DIAMOND NA RAYVAN, HATUA KALI KUCHUKULIWA DHIDI YAO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BASATA YAWAONYA DIAMOND NA RAYVAN, HATUA KALI KUCHUKULIWA DHIDI YAO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/basata-yawaonya-diamond-na-rayvan-hatua.html
0 Response to "BASATA YAWAONYA DIAMOND NA RAYVAN, HATUA KALI KUCHUKULIWA DHIDI YAO"
Post a Comment