Loading...
title : BENKI YAELEZA ILIVYOJIPANGA KATIKA KUFANIKISHA KWA VITENDO UJENZI WA TANZANIA YA VIWANDA
link : BENKI YAELEZA ILIVYOJIPANGA KATIKA KUFANIKISHA KWA VITENDO UJENZI WA TANZANIA YA VIWANDA
BENKI YAELEZA ILIVYOJIPANGA KATIKA KUFANIKISHA KWA VITENDO UJENZI WA TANZANIA YA VIWANDA
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WAKATI Serikali ya Awamu ya Tano chini Rais Dk.John Magufuli ikihimiza ujenzi wa viwanda ili kufikia uchumi wa kati, uongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesema imeweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kujenga uchumi imara utakaotokana na viwanda.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na wahariri wa habari za uchumi na biashara kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini , Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Theobard Sabi amesema wanatambua Serikali imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na kuifikisha Tanzania kuwa nchi yenye hadhi ya kipato cha kati na kuondokana na umaskini kufikia mwaka 2025.
"NBC inaunga mkono dhamira hiyo kwa kuwawezesha wafanyabiashara katika sekta mbalimbali na mitaji ya kifedha. Kama mnavyofahamu kwamba NBC ni moja ya benki yenye mtaji mkubwa wa kuwawezesha wafanyabiashara wa kitanzania. Hivyo tutahakikisha tunashiriki kikamilifu katika kuwajengea uwezo wa Tanzania ili washiriki kwenye kujenga uchumi kupitia viwanda na hayo ndio moja ya malengo yetu kama benki yenye uwezo mkubwa kifedha,"amesema Sabi.
Kuhusu vipaumbele vya benki hiyo, amesema kuwa wameweka vipaumbele vitano na namna ya kufanikisha.Amesema kipaumbele chao cha kwanza ni mteja kuwa namba moja na safari ya kumuweka mtaja kuwa wa kwanza itakazia kwenye mabadiliko ya kitamaduni ya benki yao na kuelekea kwenye utoaji hasa katika maeneo ya malipo, ufunguaji na ufufuaji wa akanti, chaneli za kidigiti pamoja na ututatuzi wa malalamiko.
Pia kipaumbele namba tatu ni kuwa karibu na wateja wao kwani NBC inaamini kwamba bila ya wateja na wao hatutakuwepo. "Hivyo tutajikita katika kuhakikisha tunakuwa karibu na wateja wetu. Tutaboresha muonekano wa matawi yetu inayoendana na matakwa na mahitaji yao.
Tumeanza na tawi letu la Dodoma ambalo lina muonekano mpya na wa kisasa unaokidhi mahitaji ya wateja wetu. Tumeanza na ukarabati wa tawi letu la Dodoma kwa sasa, lakini mengine yatafuata,"amesema Sabi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi akielezea mpango makakati wa miaka mitano wa benki hiyo wenye lengo la kuboresha kwa kiwango kikubwa huduma za benki hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea mpango mkakati wa miaka mitano wa benki hiyo wenye lengo la kufanya maboresho makubwa kwenye huduma zake. Kushoto kwake ni jopo zima la wakurugenzi wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (mbele), akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea mpango mkakati wa miaka mitano wa benki hiyo wenye lengo la kufanya maboresho makubwa kwenye huduma zake. Walioketi ni baadhi ya wakurugenzi wa NBC.
Hivyo makala BENKI YAELEZA ILIVYOJIPANGA KATIKA KUFANIKISHA KWA VITENDO UJENZI WA TANZANIA YA VIWANDA
yaani makala yote BENKI YAELEZA ILIVYOJIPANGA KATIKA KUFANIKISHA KWA VITENDO UJENZI WA TANZANIA YA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BENKI YAELEZA ILIVYOJIPANGA KATIKA KUFANIKISHA KWA VITENDO UJENZI WA TANZANIA YA VIWANDA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/benki-yaeleza-ilivyojipanga-katika.html
0 Response to "BENKI YAELEZA ILIVYOJIPANGA KATIKA KUFANIKISHA KWA VITENDO UJENZI WA TANZANIA YA VIWANDA"
Post a Comment