Loading...
title : DC Mjema ameagiza ukatili wa kingono Wamama,Watoto Kubakwa Ilala ukomeshwe
link : DC Mjema ameagiza ukatili wa kingono Wamama,Watoto Kubakwa Ilala ukomeshwe
DC Mjema ameagiza ukatili wa kingono Wamama,Watoto Kubakwa Ilala ukomeshwe
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizunngumza na Wananchi wa wilaya ya Ilala Dar es Salaam
Wananchi wa wilaya ya Ilala wakiwa katika siku ya kupinga ukatili Dar es salaam PICHA NA HERI SHAABAN
Na Heri Shaban
MKUU wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema ameagiza ukatili wa kingono katika wilaya ya Ilala wanaofanyiwa wamama,watoto wanaobakwa na wababa kuingiliwa kinyume cha maumbile vikomeshwe.
Sophia Mjema ametoa agizo hilo mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa kampeni za siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na Watoto.
"Kumekuwepo vitendo vya ukatili wa kingono, wamama wanabakwa, watoto wanabakwa na wababa kuingiliwa kinyume cha maumbile. Pia kukosekana kwa uaminifu kwa wanandoa kufanyiwa ngono bila kinga,kushikwa sehemu za Siri bila kinga, kushikwa sehemu za mwili bila makubaliano ukatili wa magonjwa Kama UKIMWI na zinaa katika wilaya yangu vikomeshwe" alisema Mjema.
Alisema kumekuwepo ukatili wa kisaikolojia ,ambapo ukatili huo umdhuru mama, Mtoto, wanaume kiakili, mfano kutukanwa ,kufokewa, kutengwa, kuzalilishwa kwa Maneno na kuhukumiwa bila kosa .
MJEMA alisema ukatili wa Kijinsia umekuwa ukiongezeka siku hadi siku taarifa nyingine zinaripotiwa na nyingine haziripotiwi hata hivyo mwanzoni tafiti nyingi zinaonyesha kwamba Wanawake na watoto ndiyo wahanga wakuu wa ukatili wa kijinsia ila kuna wababa pia ni wahanga wahanga wa kijinsia kwa sasa..
Alisema Wanawake ,watoto wanaume wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa kimwili ikiwemo kupigwa, kusukumwa, kuporwa kukeketwa kwa kipindi cha mwezi Julai hadi September 2018 kumetokea matukio ya ukatili kwa Wilaya ya Ilala Jumla kuu 126 ambapo ukatili wa kimwili 40 wanaume 10 Wanawake 30, ukatili wa kihisia au kisaikolojia Jumla 47 Wanawake 46 wanaume mmoja.
Aidha pia Mjema alielezea ukatili wa KINGONO ubakaji na ulawiti wilaya hiyo alisema kwa kipindi hicho Watu 22 walibakwa ambapo Wanawake 20 na wanaume walikuwa wawili.
Wakati huohuo Mjema alisema kumekuwa na ukatili wa kiafya kwa baadhi ya kabila,mama kukosa haki ya uzazi ya kujifungulia hospitali mume kumzuiya Mke kutumia uzazi wa Mpango.
Pia wanaume wengi wamekuwa wakipima VVU na UKIMWI na kuwaficha wakezao na wanaume wengi wanagoma kusindikizana na wake zao hospitali ili kupima afya zao kwa kisingizio kwamba ukipima wewe inatosha.
Kwa upande wake Mkuu wa Dawati POLISI Kanda Maalum Dar es salaam ASP Hellen Gardner alisema dhumuni la siku hiyo November 1960 Wanawake watatu waliuwawa kikatili na wafuasi wa kiongozi wa Jamhuri ya Dominica ambapo baada tukio hilo 1981 JAMII ya kimataifa ilianza kutambua rasmi Kama siku ya kupinga ukatili dhidi ya Wanawake.
ASP Helen alisema kauli mbiu ya mwaka huu "Funguka Usalama wake wajibu wangu kauli mbiu unatoa wito kwa kila mmoja wetu kuchukua hatua, kuhoji ,kupaza Sauti, kuwalinda Wanawake na watoto dhidi ya vitendo vya ukatili vinavyotokea Mahala pa kazi, mashuleni, mitaani, katika taasisi, hospitalini na kwenye usafiri wa Umoja.
Alisema kauli mbiu ya DAWATI la jinsia na watoto tunashawishi kila Mmoja wetu katika nafasi yake kuchukua hatua.
Hivyo makala DC Mjema ameagiza ukatili wa kingono Wamama,Watoto Kubakwa Ilala ukomeshwe
yaani makala yote DC Mjema ameagiza ukatili wa kingono Wamama,Watoto Kubakwa Ilala ukomeshwe Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC Mjema ameagiza ukatili wa kingono Wamama,Watoto Kubakwa Ilala ukomeshwe mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/dc-mjema-ameagiza-ukatili-wa-kingono.html
0 Response to "DC Mjema ameagiza ukatili wa kingono Wamama,Watoto Kubakwa Ilala ukomeshwe"
Post a Comment