Loading...

DKT. ASHATU KIJAJI AAGIZA MFANYAKAZI WA TRA DODOMA ASIMAMISHWE KAZI KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZI

Loading...
DKT. ASHATU KIJAJI AAGIZA MFANYAKAZI WA TRA DODOMA ASIMAMISHWE KAZI KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT. ASHATU KIJAJI AAGIZA MFANYAKAZI WA TRA DODOMA ASIMAMISHWE KAZI KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT. ASHATU KIJAJI AAGIZA MFANYAKAZI WA TRA DODOMA ASIMAMISHWE KAZI KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZI
link : DKT. ASHATU KIJAJI AAGIZA MFANYAKAZI WA TRA DODOMA ASIMAMISHWE KAZI KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZI

soma pia


DKT. ASHATU KIJAJI AAGIZA MFANYAKAZI WA TRA DODOMA ASIMAMISHWE KAZI KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZI



Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kumsimamisha kazi maramoja mfanyakazi wake mmoja katika Ofisi ya TRA mkoa wa Dodoma, DANIEL KINGU, kupisha uchunguzi wa kuhusika kwake na tuhuma zinazomkabili za kumbughudhi mfanyabiashara mmoja Jijini humo.

Dkt. Kijaji, ametoa maagizo hayo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kwenye mitaa ya Jiji la Dodoma baada ya kupata malalamiko kutoka kwa mfanyabiashara mmoja kwamba amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka kwa mfanyakazi huyo akishirikiana na watu wengine na kumtaka ampelekee shilingi laki 7 za kulipia mashine ya kutolea stakabadhi za kielektroniki (EFD Machine) la sivyo angefungiwa biashara yake.

“Mteja wetu awe salama!! na nitaendelea kufuatilia, lakini kuanzia muda huu Kingu aondoke ofisini, hatuwezi kuwavumilia watu wa jinsi hii hata kidogo kwa sababu kazi ya kuuza EFD machine si yake na anamwambia mteja aende ofisini kwake chumba namba fulani, anafanya haya mambo ndani ya ofisi ya Serikali, akitoka nje inakuwaje?” alihoji Dkt. Kijaji

Alisema hatasita kuchukua hatua hizo kwa wafanyakazi wengine wa Mamlaka ya Mapato popote walipo nchini wanaojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akipewa maelezo na Meneja Msaidizi upande wa Ukaguzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mustapha Mkiramweri alipofanya ziara ya kushitukiza katika mmoja wa mitaa Jijini Dodoma, kusikiliza kero za wafanyabiashara zinazoelekezwa kwenye Mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa Dodoma. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akipewa maelezo na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Thomas Masese (kulia) alipokuwa akifanya ziara ya kuwatembelea wafanyabiashara na kujua changamoto wanazokumbana nazo kutoka kwa TRA mkoani Dodoma. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akiwa na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA), wakisikiliza malalamiko ya mteja kwa njia ya simu walipomtembelea ofisini kwake kujua changamoto wanazokumbana nazo kutoka kwa TRA mkoani Dodoma, baada ya mfanyabiashara huyo kuilalamikia TRA kumlazimisha kununua mashine za kutolea stakabadhi ya kielektroniki (EFD Machine) .




Hivyo makala DKT. ASHATU KIJAJI AAGIZA MFANYAKAZI WA TRA DODOMA ASIMAMISHWE KAZI KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZI

yaani makala yote DKT. ASHATU KIJAJI AAGIZA MFANYAKAZI WA TRA DODOMA ASIMAMISHWE KAZI KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT. ASHATU KIJAJI AAGIZA MFANYAKAZI WA TRA DODOMA ASIMAMISHWE KAZI KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/dkt-ashatu-kijaji-aagiza-mfanyakazi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DKT. ASHATU KIJAJI AAGIZA MFANYAKAZI WA TRA DODOMA ASIMAMISHWE KAZI KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZI"

Post a Comment

Loading...