Loading...
title : Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa
link : Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa
Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa
Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiongea na wataalamu wa lugha ya Kiswahili ( Hawapo katika picha), jana Jijini Dodoma katika halfa ya kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67 waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) jana Jijini Dodoma
Na. Lorietha Laurence-WHUSM,Dodoma
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa lugha ni kielelezo na sehemu muhimu ya utambulisho wa taifa lolote duniani.
Hayo ameyasema jana Jijini Dodoma katika Hafla ya kuwatunuku vyeti vya utambuzi wataalamu 67 wa lugha ya Kiswahili waliofuzu mafunzo ya muda mfupi yaliyoandaliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).
“Taifa lolote lisilo na utamaduni wake ni taifa mfu, na sisi tunajivunia kwa kuwa na utamaduni hai ikiwemo lugha yetu ya Kiswahili” alisema Dkt. Mwakyembe
Aidha aliongeza kwa kueleza kuwa lugha ya Kiswahili ni kitambulisho cha utamaduni wa Mtanzania , kwa kuwa ndiyo lugha inayowaunganisha watu katika shughuli mbalimbali za Kijamii, Kisiasa na kiuchumi.
Dkt. Mwakyembe anazidi kufafanua kuwa takribani lugha elfu sita (6000) huzungumzwa kila siku duniani ambapo lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa lugha 10 zinazoongelewa kwa wingi.
“Mafunzo haya ni mwanzo tu mwa mambo mengi mazuri ambayo Wizara yangu imepanga kufanikisha na ukizingatia kampeni ya mwaka huu ya Uzalendo na Utaifa ina kauli mbiu inayohamasisha kukuza lugha yetu ambayo ni Kiswahili Utashi Wetu, Uhai Wetu” alisema Dkt. Mwakyembe.
Naye Kaimu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Bibi. Consolata Mushi alieleza kwamba mpaka sasa Baraza limefanikiwa kutoa mafunzo kwa wataalamu 350 ambapo jumla ya wataalamu wapatao 198 tayari wametunukiwa vyeti na wataalamu 98 wanatarajiwa kutunukiwa vyeti hivyo mwezi Desemba 2018.
Anazidi kueleza kuwa lengo la BAKITA ni kuwapa fursa wataalamu hao ili waweze kusajiliwa katika mfumo wa kanzi data ambayo tayari imesajili wataalamu wapatao 380 kwa ajili ya kufundisha lugha ya Kiswahili kwa wageni ndani na nje ya nchi.
Pia Bibi. Consolata alitoa wito kwa wataalamu wa Kiswahili kutoka katika mikoa yote ya Tanzania Bara kujiunga na kupata mafunzo hayo ili waweze kuorodheshwa katika kanzi data hiyo kwa ajili ya kukibidhaisha Kiswahili katika mataifa mengine.
Kwa niaba ya wahitimu wenzake Mwalimu wa shule ya Sekondari Chikole ya Jijini Dodoma Bibi. Neema Mkobalo alimshukuru Waziri Dkt. Mwakyembe pamoja na uongozi wa BAKITA kwa kuratibu mafunzo hayo na kuahidi kufanyia kazi yale yote waliyojifunza .
Hivyo makala Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa
yaani makala yote Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/dkt-mwakyembe-lugha-ni-kielelezo-cha_3.html
0 Response to "Dkt. Mwakyembe-Lugha ni Kielelezo cha Taifa"
Post a Comment