Loading...
title : jamii yashauriwa kutilia mkazo malezi ya kiuchumi na elimu ya ujasiriamali
link : jamii yashauriwa kutilia mkazo malezi ya kiuchumi na elimu ya ujasiriamali
jamii yashauriwa kutilia mkazo malezi ya kiuchumi na elimu ya ujasiriamali
Mwamba wa habari
Jamii imeshauriwa kuacha utamaduni wa kuyakimbia majukumu ya malezi ya kiuchumi badala yake ijikite katika kutoa eliumu ya ujasiriamali kwa watoto itakayosaidia kuwakomboa kiuchumi pamoja na kuliingizia taifa kipato.
Aidha, wazazi wametakiwa kuacha kuegemea kuchangia sherehe za harusi badala yake wajikite kutoa msaada wa kiuchumi kwa watoto wao wanaoshiriki harusi hizo kuwakwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Joseph Kakunda katika Maonesho ya Ujasiriamali kwa vijana yaliyoandaliwa na Taasisi ya Nama inayojishughulisha na masuala ya utoaji elimu ya ujasiriamali kwa vijana na kuwawezesha kupitia mikopo nafuu.
Amesema kuwa kuna utamaduni umejenga katika jamii ambapo wazazi hutumia fedha nyingi kwenye sherehe za harusi za watoto na kwamba baada ya harusi wanandoa huishi magumu kutokana kutowezeshwa kiuchumi.
" Jamii isikimbie malezi ya kiuchumi kwa watoto tuwape elimu ya ujasiriamali tusiishie katika kuchangia harusi baada ya harusi tukawaacha watoto kwenye hali ngumu," amesema waziri Kakunda.
Amebainisha kuwa vijana wamekuwa wakishindwa fursa za mikopo sababu ya kutopewa elimu sahihi ya njia za kupitia na kusisitiza wakati wengine hukwamishwa na watu wasiohusika nadni ya taasisi husika.
Amesisitiza kuwa tayari ameshaiagiza Sido kutangaza fursa walizonazo ili vijana na watu wenye nia ya kupata mikopo wachangamkie fursa hiyo na kwa kila wilaya imetengwa sh bilioni 8 za mikopo kwa wahitaji
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa taasisi hiyo,Musa Msingwa amesema hadi sasa wameshawafikia vijana 130 ambao wamepewa elimu ya kutambua na kuchangamkia fursa zilizopo.
Amefafanua kuwa wana mikakati madhubuti ya kuhakikisha wanawafikia vijana wengine katika mikoa mingine ukiwemo mkoa wa Mtwara.
Naye mshiriki wa maonesho hayo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Matatu Enterprises, Hussein Abeid ameiomba Serikali kuendelea kutoa mitaji kwa wajasiriamali waweze kutafuta masoko ya uhakika na kujitangaza.
Hivyo makala jamii yashauriwa kutilia mkazo malezi ya kiuchumi na elimu ya ujasiriamali
yaani makala yote jamii yashauriwa kutilia mkazo malezi ya kiuchumi na elimu ya ujasiriamali Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala jamii yashauriwa kutilia mkazo malezi ya kiuchumi na elimu ya ujasiriamali mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/jamii-yashauriwa-kutilia-mkazo-malezi.html
0 Response to "jamii yashauriwa kutilia mkazo malezi ya kiuchumi na elimu ya ujasiriamali"
Post a Comment