Loading...

KASI ZAIDI YATAKIWA KUSIMAMIA SEKTA YA UVUVI

Loading...
KASI ZAIDI YATAKIWA KUSIMAMIA SEKTA YA UVUVI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa KASI ZAIDI YATAKIWA KUSIMAMIA SEKTA YA UVUVI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : KASI ZAIDI YATAKIWA KUSIMAMIA SEKTA YA UVUVI
link : KASI ZAIDI YATAKIWA KUSIMAMIA SEKTA YA UVUVI

soma pia


KASI ZAIDI YATAKIWA KUSIMAMIA SEKTA YA UVUVI


Na. Edward Kondela

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amekutana na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma, Mjini Unguja na kumweleza kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inahakikisha miradi inayohusu wavuvi inawanufaisha moja kwa moja.

Katika mazungumzo hayo ambayo pia yamehudhuriwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Makame Ali Ussi, Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Bw. Islam Seif Salum pamoja na watendaji wengine wizara, Mhe. Ulega amesema lengo kuu la ziara yake ya siku moja kisiwani Zanzibar ni kutazama shughuli za Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Kuu Zanzibar kupitia mradi wa Usimamizi wa Uvuvi Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi (SWIOFISH).

“Tunahitaji tuone rasilimali za bahari zinatunufaisha, mchango wake bado ni mdogo sana mradi wa SWIOFISH una pesa nyingi lakini bado hatujaona mafanikio ya moja kwa moja kuwasaidia wananchi tulikubaliana kuna mambo ya kurekebisha.” Alisema Mhe. Ulega

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma amesema uchafuzi wa bahari, uwepo wa maharamia na uvuvi haramu ni mambo ambayo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea kukabiliana nayo ili kuhifadhi bahari na kufanya sekta ya uvuvi kuwa yenye tija kwa wananchi.

Mhe. Juma pia amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika masuala yanayohusu uvuvi ili kubadilishana uzoefu hasa baada ya hivi karibuni kuhudhuria mkutano wa “Blue Economy” nchini Kenya ambapo nchi washiriki wa mkutano huo walikubaliana kusimamia mambo mbalimbali ili kulinda rasilimali za Bahari ya Hindi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) akiwa na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma.





Hivyo makala KASI ZAIDI YATAKIWA KUSIMAMIA SEKTA YA UVUVI

yaani makala yote KASI ZAIDI YATAKIWA KUSIMAMIA SEKTA YA UVUVI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala KASI ZAIDI YATAKIWA KUSIMAMIA SEKTA YA UVUVI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/kasi-zaidi-yatakiwa-kusimamia-sekta-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "KASI ZAIDI YATAKIWA KUSIMAMIA SEKTA YA UVUVI"

Post a Comment

Loading...