Loading...

Manispaa ya Ilala wazindua Jukwaa la Vijana

Loading...
Manispaa ya Ilala wazindua Jukwaa la Vijana - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Manispaa ya Ilala wazindua Jukwaa la Vijana, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Manispaa ya Ilala wazindua Jukwaa la Vijana
link : Manispaa ya Ilala wazindua Jukwaa la Vijana

soma pia


Manispaa ya Ilala wazindua Jukwaa la Vijana


OFISA Vijana wa Manispaa ya Ilala Sapiencia MASAGA akimkabidhi Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ilala Jabir Makame taarifa ya uzinduzi wa Jukwaa la Vijana Manispaa ya Ilala Dar es Salam leo PICHA NA HERI SHAABAN

Na Heri Shaban
MANISPAA ya Ilala wamezindua Jukwaa la Vijana kwa ajili ya kupanga Mikakati na kupeana fursa za Maendeleo katika manispaa hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi huo Wilayani Ilala Dar es Salam leo, Ofisa Tarafa wilaya ya Ilala, Jabir Makame ambaye alimwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo alisema  uzinduzi wa Jukwaa hilo la Vijana Manispaa ya Ilala itakuwa sehemu muhimu kwa vijana wa manispaa ya Ilala kupashana habari za uwepo wa fursa mbalimbali zinazowagusa ili kujiletea Maendeleo yao wenyewe kwa Jamii inayowazunguka na TAIFA kwa Jumla.

Jabir alipongeza Manispaa ya Ilala kupitia idara ya Maendeleo ya Jamii  kwa uwezo wake mkubwa wa kuihudumia Jamii ya vijana kwa mafanikio yaliopatikana kwa kipindi cha mwaka 2017/2018.

"Suala la kuhudumia vijana huchangiwa na utekelezaji wa Sera mbalimbali hasa sera za sekta zilizo kubwa ambazo zimechangia muonekano wa hali ya vijana kwa sasa "alisema Makame.

Makame alisema pamoja na uwepo wa changamoto za kitaifa na kidunia katika kuwahudumia kama vile kujitokeza katika masuala mapya ya kitaifa na kidunia ambayo ni mabadiliko ya mtindo wa maisha,kuibuka kwa tamaduni mpya na changamoto nyingine  kama zilivyoelezwa  kwenye taarifa ndio sababu ya vijana wa kike na kiume kukosa mwelekeo kupelekea kufanya mambo yasiyo faa katika JAMII.

Aliwapongeza wadau wa Maendeleo ya vijana kwa jitihada zao katika kuakikisha nguvu kazi kubwa ya Vijana inaleta mageuzi ya kijami, kiuchumi, na kitamaduni, kwa kupitia afua mbalimbali mnazozitekeleza katika maeneo ya Manispaa ya Ilala.

Aidha Jabir alisema kwa kufanya hivyo wanatekeleza sera ya TAIFA ya Maendeleo ya Vijana ya Mwaka 2007 na ILANI ya Uchaguzi kwa vitendo.

Kwa upande wake Ofisa Vijana wa Manispaa ya Ilala Sapiencia Masaga,alisema Halmashauri ya Ilala kupitia sehemu ya vijana iliyopo Idara ya Maendeleo ya Jamii ina jukumu la kutoa huduma ya Vijana ambazo ni pamoja na Kuunda vikundi vya ujasiriamali na utoaji wa mikopo, utoaji wa elimu ya Afya ya uzazi, stadi za maisha na ujasiriamali, utoaji wa elimu ya madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya na kuunda vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi  kama DADA Poa na Kaka Poa.

MASAGA alisema kwa Mwaka wa fedha 2017/2018 imefanikiwa  kutoa mikopo kupitia mfuko wa Halmashauri (IWYDF)jumla ya Vijana 8,482 Wamenufaika kwa kuongeza Mitaji katika Biashara zao kwa kushirikiana na SACCOS ya VIJANA ya Manispaa ambapo jumla ya vikundi 12 imenufaika kwa kupata mikopo ya Wizara  .

Pia VIJANA 126 walipata mafunzo ya Wajasiriamali na kujiajiri kupitia asasi ya TECC wanatekeleza Mradi wa "kijana -Via Jiandalie Ajira,kutoa elimu ya madhara ya Matumizi ya madawa ya kulevya kwa Vijana 2720 kupitia asasi ya Yovalibe na mkikute kwa kushirikiana na asasi ya CAFLO    kwa kutoa elimu kwa njia mbalimbali.

  Dhumuni la kongamano hilo la Jukwaa la Vijana (Ilala Youth Forum -IYF) lina umuhimu pekee kwa kuwakutanisha kwa mara ya kwanza wawakilishi wa Vijana kutoka kata zote za MANISPAA ya Ilala na Wadau wa Maendeleo na kuwawezesha kubadilishana uzoefu na mbinu mpya katika kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika kuleta Maendeleo.

Alisema kulingana na matokeo ya sensa ya Mwaka 2012 yalionyesha kuwa asilimia 77 ya watu wenye umri wa miaka 15 hadi 35 Tanzania ni Vijana ambao ndio nguvu kazi ya TAIFA wengi wao Wajasiriamali wadogo na wa kati.

Naye Mkurugenzi wa Ilala Jumanne Shauri alisema Manispaa yake imetenga shilingi bilioni 1 ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kwa ajili ya utoaji mikopo pia shilingi milioni 670 ndio wanaanza kuwapa mikopo vikundi vilivyopo Manispaa Ilala.




Hivyo makala Manispaa ya Ilala wazindua Jukwaa la Vijana

yaani makala yote Manispaa ya Ilala wazindua Jukwaa la Vijana Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Manispaa ya Ilala wazindua Jukwaa la Vijana mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/manispaa-ya-ilala-wazindua-jukwaa-la.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Manispaa ya Ilala wazindua Jukwaa la Vijana"

Post a Comment

Loading...