Loading...
title : Manispaa ya Ubungo kujenga ofisi ya bilioni 6.2
link : Manispaa ya Ubungo kujenga ofisi ya bilioni 6.2
Manispaa ya Ubungo kujenga ofisi ya bilioni 6.2
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, imesaini mkataba wa Bilioni 6.2 kwa ajili ya ujenzi wa jengo kisasa la Utawala la Halmashauri hiyo litakalojengwa na wakala wa Majengo Nchini (TBA). Akizungumza wakati wa utiaji saini ujenzi wa jengo hilo la Utawala leo jijini Dar es Salaam, Meya Jacob amesema ni matarajio yake ujenzi huo utakamilika kwa wakati kama walivyopanga katika kuondokana na ofisi za kupanga
Amesema Serikali Kuu ilitoa mwongozo wa kuhakikisha wanawatumia TBA katika mradi huo lakini angekuwa yeye binafsi angependekeza kushindanisha wakandarasi kadhaa wakiwamo Suma JKT ili kupata mkandarasi mwingine. "Naomba nitoe tahadhali kwa TBA mkajipime kabl hamjaanza ujenzi huu kwani mkionyesha kusuasua mimi ndio ntakuwa wa kwanza kulalama kwa vile wadau wetu wa pili wa mradi huu ambao ni Serikali wamewateua nyie mjitahidi msiwaangishe ili kuendelea kuwa na imani na nyie" amesema Jacob.
Aliweka angalizo hilo kwa sababu ya historia fupi ya TBA kwenye baadhi ya mikoa ambapo wameshindwa kutekeleza mikataba na kusababisha mingine kunyang'anywa. "Tumeskia huko mikoani baadhi ya miradi mliporwa kwa sababu ya uzembe wa watendaji wenu wa huko lakini kwa hapa Dar ea Salaam hamjapata kashfa hiyo hivyo naomba mjipange vyema katika mradi huu kwa kufanya kuwa na jengo,"alisema Jacob.
Mkuregenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Kwai(kulia) na Meneja wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA) Mkoa wa Dar es Salaam, Edwin Godfrey(kushoto) wakibadilishana hati za makubaliano ya ujenzi ofisi ya manispaa hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob.(Picha na Emmanuel Massaka wa MMG)Meya wa Manispaa ya Ubungo Boniface Jacob akizungumza na waandishi habari mara baada kutiliana saini ya makubaliano ya ujenzi wa Manispaa hiyo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuregenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Kwai na kushoto ni Meneja wa Wakala wa Majengo Nchini (TBA) Mkoa wa Dar es Salaam, Edwin Godfrey.
TBA na Manispaa ya Ubungo wakisaini Mkataba ya makubaliano ya ujenzi wa Manispaa hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Kwai akizungumza na waandishi habari namna waliyojiwekea mazingira ya ujenzi wa Manispaa hiyo wakati wa kuliliana saini na TBA.
Picha ya pamoja ya watendaji na Manispaa ya Ubungo na TBA na baadhi ya Madiwani
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Manispaa ya Ubungo kujenga ofisi ya bilioni 6.2
yaani makala yote Manispaa ya Ubungo kujenga ofisi ya bilioni 6.2 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Manispaa ya Ubungo kujenga ofisi ya bilioni 6.2 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/manispaa-ya-ubungo-kujenga-ofisi-ya.html
0 Response to "Manispaa ya Ubungo kujenga ofisi ya bilioni 6.2"
Post a Comment