Loading...
title : MSHAMBULIAJI SIMBA AFUNGUKA LIGI YA MABIGWA AFRIKA.
link : MSHAMBULIAJI SIMBA AFUNGUKA LIGI YA MABIGWA AFRIKA.
MSHAMBULIAJI SIMBA AFUNGUKA LIGI YA MABIGWA AFRIKA.
Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Simba, Mzambia, Clatous Chota Chama, amefunguka machache kuhusiana na moja ya bao alilolifunga dhidi ya Mbabane Swallows katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Chama ameandika kuwa hawezi kuchoka kulitazama bao alilofunga huku akimwomba Mungu azidi kuwapa nguvu ya kufuzu pia hatua ijayo.
“Siwezi kuacha kulitazama hili bao asante Mungu kwa kunipa nafasi ya kufunga na kuifanya Simba iweze kufanikiwa kwenda hatua nyingine katika michuano hii ya Caf mimi pamoja na wachezaji wenzagu,” alisema Chama.
“Hivyo, basi ninataka kuona timu yangu inafika katika hatua nzuri ya michuano hii mikubwa Afrika na hilo linawezekana kabisa kwa kushirikiana na wenzangu,” alisema Chama.
Juzi katika mitandao mbalimbali za Zambia gumzo ilikuwa ni Chama huku Nkana wakionywa kuwa nae makini.
Chama tayari ana mabao matatu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika huku Bocco na Kagere kila mmoja akiwa na mabao mawili
Hivyo makala MSHAMBULIAJI SIMBA AFUNGUKA LIGI YA MABIGWA AFRIKA.
yaani makala yote MSHAMBULIAJI SIMBA AFUNGUKA LIGI YA MABIGWA AFRIKA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MSHAMBULIAJI SIMBA AFUNGUKA LIGI YA MABIGWA AFRIKA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/mshambuliaji-simba-afunguka-ligi-ya.html
0 Response to "MSHAMBULIAJI SIMBA AFUNGUKA LIGI YA MABIGWA AFRIKA."
Post a Comment