Loading...

Mwakyembe kuona kijiji cha wasanii Mkuranga

Loading...
Mwakyembe kuona kijiji cha wasanii Mkuranga - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mwakyembe kuona kijiji cha wasanii Mkuranga, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mwakyembe kuona kijiji cha wasanii Mkuranga
link : Mwakyembe kuona kijiji cha wasanii Mkuranga

soma pia


Mwakyembe kuona kijiji cha wasanii Mkuranga

WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo,Harrison Mwakyembe amekubali mwaliko wa kutembelea kijiji cha wasanii Mwanzega kujionea maendeleo ya ujenzi wa nyumba za wasanii.

Katibu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Michael Kagondela akizungumza jana wakati wa hafla ya  kukabidhi nyumba 15 kwa wasanii na wanamichezo alisema katika mazungumzo ya SHIWATA na Waziri Mwakyembe kuomba kijiji chao chenye nyumba za makazi kutambuliwa wizarani yamefanikiwa.

"Nawataarifuni kuwa SHIWATA inafanya kazi zake kwa uwazi na kufuata taratibu za kiserikali, tumemuomba Waziri Mwakyembe atutembelee na yeye amekubali kuja hapa kijijini kwetu huo ni ugeni uliopo mbele yetu "alisema Kagondela. Mmoja kati ya waliokabidhiwa nyumba hizo Mwanabaraka Mchinga alishukuru kukabidhiwa nyumba yenye thamani ya sh. Mil. 4.3 alizochangia kidogo kidogo mpaka kukamilisha kiasi hicho na kukabidhiwa nyumba yake.

Mwanachama mwingine anayeishi kijijini hapo Monica Humba alisema ameona mafanikio makubwa kutoka ahamie kijiji cha wasanii kwa sababu anaishi maisha ya gharama ya chini kwa sababu kila kitu analima na kufuga mwenyewe. Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwanzega, Kitongoji cha Gomapembe Seif Katundu aliwashauri wasanii kuwekeza kijijini kwa kumalizia ujenzi wa nyumba kwa vile Serikali ya awamu  ya tano ni sikivu itatekeleza kero zote za wananchi wake za maji,barabara na zahanati.

SHIWATA ambayo mbali ya kuendesha matamasha ya wasanii wa fani mbalimbali pia inajenga nyumba kwa wanachama wake na kumiliki shamba la ekari 220 katika kijiji cha Ngarambe wilayani Mkuranga. Wakati huo huo uchaguzi wa viongozi wa SHIWATA utafanyika Januari 19,2019 kama ulivyopangwa awali na fomu zitaendelea kutolewa na kurudishwa mpaka Januari 4, mwakani ni mwisho.


Hivyo makala Mwakyembe kuona kijiji cha wasanii Mkuranga

yaani makala yote Mwakyembe kuona kijiji cha wasanii Mkuranga Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mwakyembe kuona kijiji cha wasanii Mkuranga mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/mwakyembe-kuona-kijiji-cha-wasanii.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mwakyembe kuona kijiji cha wasanii Mkuranga"

Post a Comment

Loading...