Loading...
title : RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU MSTAAFU WA USALAMA WA TAIFA, BW. APSON MWANG’ONDA
link : RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU MSTAAFU WA USALAMA WA TAIFA, BW. APSON MWANG’ONDA
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU MSTAAFU WA USALAMA WA TAIFA, BW. APSON MWANG’ONDA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Desemba, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw. Apson Mwang’onda, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Baada ya mazungumzo hayo Bw. Apson Mwang’onda amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kukubali ombi lake la kumuona na kuzungumza naye na amempongeza kwa uongozi mzuri unaochochea kasi ya maendeleo hususani katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.
Bw. Apson Mwang’onda ameitaja baadhi ya miradi mikubwa ya maendeleo kuwa ni mradi wa uzalishaji wa umeme katika mto Rufiji (Stieglers’ Gorge Power Project) na Ujenzi wa madaraja na barabara ambazo licha ya kurahisisha usafiri zitasaidia kuondoa msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.
“Mabadiliko ni makubwa sana ambayo yametokea, kuna miradi mikubwa mingi inafanyika sasa hivi, kwa hiyo mabadiliko ni makubwa kusema kweli na yote hayo ni kwa manufaa ya nchi, kwa hiyo nachoweza kusema amefanya kazi kubwa kwa maendeleo ya nchi” amesema Bw. Apson Mwang’onda.
Ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Awamu ya Tano ili itekeleze mipango yake kwa ufanisi na kwa manufaa ya Taifa.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Desemba, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw. Apson Mwang’onda Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, alipomtembela Ikulu jijini Dar es Salaam.Disemba 6,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Bw. Apson Mwang’onda Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, wakati wanaagana mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.Disemba 6,2018.
Hivyo makala RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU MSTAAFU WA USALAMA WA TAIFA, BW. APSON MWANG’ONDA
yaani makala yote RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU MSTAAFU WA USALAMA WA TAIFA, BW. APSON MWANG’ONDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU MSTAAFU WA USALAMA WA TAIFA, BW. APSON MWANG’ONDA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/rais-dkt-magufuli-akutana-na-kufanya.html
0 Response to "RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKUU MSTAAFU WA USALAMA WA TAIFA, BW. APSON MWANG’ONDA"
Post a Comment