Loading...

RAIS DKT.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM ZANZIBAR

Loading...
RAIS DKT.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM ZANZIBAR - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RAIS DKT.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM ZANZIBAR, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RAIS DKT.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM ZANZIBAR
link : RAIS DKT.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM ZANZIBAR

soma pia


RAIS DKT.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM ZANZIBAR

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar  ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo ameongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar. Kikao hicho cha Siku Moja kimeanza majira ya saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar na kuhudhuriwa na Wajumbe wa Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Zanzibar.

Kupitia Kikao hicho  Makamu Mwenyekiti Dk. Ali Mohamed Shein, aliwapongeza Wanachama, Watendaji na Viongozi wote wa CCM kwa kufanikisha Ushindi wa kishindo katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang’ombe ambapo aliyekuwa Mgombea wa CCM Mhe.Ramadhan Hamza Chande alishinda kwa  kura 7,274 sawa na asilimia 90.5.

Dk.Shein alieleza kuwa ushindi huo haukuwa wa bahati mbaya bali ulitokana na ridhaa ya Wananchi wa Jimbo hilo kwa kuridhishwa na kasi ya Utekelezaji kwa vitendo Sera na mipango endelevu ya maendeleo inayotekelezwa kupitia Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.

Katika maelezo yake Dk.Shein aliwasisitiza Wajumbe wa Kikao hicho na Wana CCM kwa ujumla kuwa Ushindi wa CCM Jang’ombe ni sehemu ya maandalizi ya Ushindi wa Kihistoria katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

WAJUMBE wa Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa ambao pia ni Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia), Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Saada Mabodi(wa kwanza kulia) , Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Idd (wa kwanza kushoto), Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto), wakiimba mara baada ya kuingia katika Ukumbi wa Mikutano wa Kamati Maalum ya NEC CCM Taifa Kisiwandui Zanzibar.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd (kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi (kulia) mara baada ya kuwasili Kisiwandui kwa ajili ya Kikao cha Kamati Maalum.(Picha na Hussein Khamis na Thani Mosi).

WAJUMBE wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar wakiwa katika Kikao cha kawaida kinachofanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu, huko Kisiwandui Afisi Kuu Zanzibar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA





Hivyo makala RAIS DKT.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM ZANZIBAR

yaani makala yote RAIS DKT.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RAIS DKT.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM ZANZIBAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/rais-dktshein-aongoza-kikao-cha-kamati.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "RAIS DKT.SHEIN AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM ZANZIBAR"

Post a Comment

Loading...