Loading...
title : SEMINA ELEKEZI YATOLEWA KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA,
link : SEMINA ELEKEZI YATOLEWA KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA,
SEMINA ELEKEZI YATOLEWA KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA,
NI KUHUSIANA NA MRADI WA UTAMBUZI WA WASANII WA SANAA ZA UFUNDI KWENYE KATA NA MITAA YAO .
Watendaji hao kutoka Kata ishirini, na mitaa yake 106, leo wameshiriki semina elekezi ya siku moja yenye lengo la kuutambulisha mradi wa utambuzi wa wasanii wa sanaa za ufundi kutoka shirika lisilo la kiserikali la TACIP, unaotarajia kuanza tarehe 19/12/2018, utakaohusisha watendaji wa kata na mitaa kwa zoezi hilo, hadi kukamilika kwake.
Akiutambulisha mradi huo, kwa watendaji wa Kata na Mitaa, Profesa Fredric Mtenzi kutoka shirika hilo amesema, lengo ni kuwapatia kadi za umeme(elektronic cards) zitakazowasogeza karibu na fursa zilizopo baada ya kutambuliwa kuorodheshwa na kuhakikiwa katika mfumo wa wasanii wa sanaa za ufundi na uchongaji.
"Kundi hili la wasanii wa sanaa za ufundi ni kundi kubwa, ambalo kwa namna moja ama nyingine linachangia kiasi kikubwa cha pato la Serikali, hivyo ni lazima nao watengenezewe fursa zitakazowasaidia katika kufanikisha shughuli zao za kila siku katika ujenzi wa Taifa" Amefafanua Prof.Mtenzi.
Akifungua semina hiyo iliyofanyika katia ukumbi wa shule ya Msingi Oysterbay Bi Pili Ngarambe kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni amesema sanaa ni ajira, hivyo kwa kuwatambua wasanii wa sanaa za ufundi, ni kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa kati wa viwanda, kwani azma yake kubwa ni kuona wananchi wanajishughulisha, na kuhakikisha kila mwenye kipaji chake anatambuliwa na kuthaminiwa, na kuwataka watendaji wa Kata na Mitaa kuwa sehemu ya zoezi hilo, ili liweze kufikiwa kusudi lililokusudiwa.
Naye Rais wa shirikisho la sanaa za ufundi Tanzania Ndg Adrian Nyangamale alipotakiwa kuzungumzia faida za mradi huu wa utambuzi wa wasanii amesema si tu sanaa yako kujulikana bali pia ni kutambulika na mamlaka za nchi, kupatiwa utatuzi wa changamoto katika fani hiyo, ni kujiongezea fursa lukuki za mafunzo na pia kupata masoko ya uhakika ya ndani na nje ya nchi.
Nyingine ni kupata malighafi na vitendea kazi kwa urahisi, kuwepo na utetezi wa haki na maslahi pamoja na kupata fursa ya kukopesheka, na kuainisha makundi ya wasanii hao kuwa ni wachoraji,wapiga picha bunifu,wachongaji, wanasanaa za mikono, wabunifu na wanasanaa jumuishi.
Kadhalika, Katibu Mtendaji Mkuu kutoka BASATA ndugu Godfrey Mngereza ameainisha jukumu kubwa walilonalo Serikali kuwa ni kuhakikisha wasanii wa sanaa za ufundi wanatumia sanaa yao ipasavyo katika jamii inayowazunguka si tu kujitafutia kipato bali pia ni kuelimisha kuburudisha, kuonya bila kuvunja sheria za Nchi.
Semina iliyoratibiwa na, Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Kinondoni Bi.Joyce Kiriho, imepata uwakilishi kutoka mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo ni Data vision, TAFCA, TACIP, na watendaji wa Kata na Mitaa yote ya Kinondoni.
Imeandaliwa na
Kitengo cha Uhusiano na Habari.
Manispaa ya Kinondoni.
Hivyo makala SEMINA ELEKEZI YATOLEWA KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA,
yaani makala yote SEMINA ELEKEZI YATOLEWA KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA, Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SEMINA ELEKEZI YATOLEWA KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA, mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/semina-elekezi-yatolewa-kwa-watendaji.html
0 Response to "SEMINA ELEKEZI YATOLEWA KWA WATENDAJI WA KATA NA MITAA,"
Post a Comment