Loading...
title : SERIKALI YATOA MBINU MPYA SIMBA, MTIGWA KUFUZU HATUA YA MAKUNDI KIMATAIFA
link : SERIKALI YATOA MBINU MPYA SIMBA, MTIGWA KUFUZU HATUA YA MAKUNDI KIMATAIFA
SERIKALI YATOA MBINU MPYA SIMBA, MTIGWA KUFUZU HATUA YA MAKUNDI KIMATAIFA
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo imetoa ushauri kwa klabu za Simba na Mtibwa kujipanga vema kuelekea mechi za marejeano za mashindano ya kimataifa.
Kupitia Waziri mwenye dhamani, Harisson George Mwakyembe, amesema kupoteza katika mechi za kwanza ambazo walicheza ugenini isiwe sababu ya kukata tamaa mapema.
Mwakyembe amewamua kuwapa nguvu Simba na Mtibwa ili waweze kujipanga vizuri kuelekea mechi za marejeano akiamini lolote linaweza kutokea ndani ya dakika 90.
"Nawasihi vijana wetu wapambane na wajipange kuelekea mechi za marudiano, sikutegemea kama wangeweza kupoteza kulingana na namna walivyofanya vizuri katika mechi za kwanza" alisema.
Katika mchezo ambao Simba walicheza dhidi ya Nkana Red Devils ya Zambia walipoteza kwa jumla ya mabao 2-1 kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Mtibwa akipoteza kwa mabao 3-0 kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Simba itarejeana na Nkana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Disemba 23 sambamba na Mtibwa ambayo watacheza na KCCA pale Azam Complex tarehe sawa na mechi ya Simba
Hivyo makala SERIKALI YATOA MBINU MPYA SIMBA, MTIGWA KUFUZU HATUA YA MAKUNDI KIMATAIFA
yaani makala yote SERIKALI YATOA MBINU MPYA SIMBA, MTIGWA KUFUZU HATUA YA MAKUNDI KIMATAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YATOA MBINU MPYA SIMBA, MTIGWA KUFUZU HATUA YA MAKUNDI KIMATAIFA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/serikali-yatoa-mbinu-mpya-simba-mtigwa.html
0 Response to "SERIKALI YATOA MBINU MPYA SIMBA, MTIGWA KUFUZU HATUA YA MAKUNDI KIMATAIFA"
Post a Comment