Loading...
title : SERIKALI YAWAAHIDI WAKAZI WA MWAPEMBA KUWAJENGEA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI
link : SERIKALI YAWAAHIDI WAKAZI WA MWAPEMBA KUWAJENGEA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI
SERIKALI YAWAAHIDI WAKAZI WA MWAPEMBA KUWAJENGEA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi ameahidi kujenga kwa kiwango cha lami barabara itokayo kwa fundi baiskeli hadi Shule ya Awali na Msingi Katavi iliyopo mtaa wa Mwapemba yenye urefu wa kilometa 1.5.
Mwakabibi alitoa ahadi hiyo mwishoni mwa wiki alipohudhuria hafla ya mahafali ya pili ya shule hiyo, kufuatia ombi lililotolewa na Mkurugenzi wa Shule hiyo, Geophrey Pinda.
Akiwasilisha ombi hilo, Pinda alisema miongoni mwa changamoto inayoikabili wananchi wa eneo hilo ni pamoja na ubovu wa barabara na kutokuwa na usafiri za daladala kutoka Barabara Kuu ya Kigamboni hadi Mwapemba.
“Kipindi cha mvua nyingi barabara yetu iliharibika sana na hivyo kuwa ngumu kupitika, tunashukuru hivi karibuni Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) walikuja kufanya matengenezo na kusawazisha mashimo makubwa yaliyokuwapo”.
“Barabara hii ambayo inapita Mtaa wa Ponde na Mwapemba ina wastani wa kilometa 1.5 ni ya muhimu kwa wakazi zaidi ya 1,000 waishio eneo hili, tuna shule mbili katavi, Ocean View pamoja na chuo cha afya ambacho hivi sasa kina wana chuo zaidi ya 2,000.
“Hivyo, tunaomba upendeleo ijengwe kiwango cha lami ikiwa inawezekana ili kutatua tatizo la usafiri linalotukabili.
“Aidha, tunayo Zahanati ya Mikwambe, tunahitaji ipandishwe hadhi ili tupate huduma saa 24, kwani sasa hivi watumishi hawawezi kufanya hivyo kwa kuwa si kituo cha afya,” alisema.
Akizungumza Mwakabibi alisema ujenzi huo utaanza wakati wowote kuanzia sasa kwani utasaidia kurahisisha maisha ya wakazi wa eneo hilo.
“Ni wazi kwamba wakazi wa eneo hili hivi sasa wanahitaji barabara imara iliyojengwa kwa kiwango cha lami, nipo tayari kusimamia hilo na hatua inaanza mara moja kuanzia sasa, lazima ijengwe katika kiwango cha lami,” alisema.
Sambamba na hilo alimuagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kufika katika zahanati hiyo ya Mikwambe kwa ajili ya kufanya tathmini.
“Nataka aje aangalie iwapo zahanati hii inastahili kupandishwa hadhi, atawasilisha ripoti yake ofisini kwangu, tutakaa na madiwani kuzungumza tuone namna tutakavyofanya ili kuipandisha hadhi, wananchi wapate huduma bora za afya wakati wote,” alisema.
Hivyo makala SERIKALI YAWAAHIDI WAKAZI WA MWAPEMBA KUWAJENGEA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI
yaani makala yote SERIKALI YAWAAHIDI WAKAZI WA MWAPEMBA KUWAJENGEA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAWAAHIDI WAKAZI WA MWAPEMBA KUWAJENGEA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/serikali-yawaahidi-wakazi-wa-mwapemba.html
0 Response to "SERIKALI YAWAAHIDI WAKAZI WA MWAPEMBA KUWAJENGEA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI"
Post a Comment