Loading...
title : TANZANIA YAANGUKIA KUNDI A FAINALI ZA AFCON U17 MWAKANI
link : TANZANIA YAANGUKIA KUNDI A FAINALI ZA AFCON U17 MWAKANI
TANZANIA YAANGUKIA KUNDI A FAINALI ZA AFCON U17 MWAKANI
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Fainali za mabingwa Afrika kwa vijana chini ya Miaka 17 (AFCON) yanayotarajiwa kufanyika Nchini Tanzania April 2019 yamefikia katika upangaji wa makundi.
Droo hiyo iliyochezeshwa jioni ya leo ikishuhuduwa na viongozi mbalimbali wa Kiserikali wakiongozwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe na viongozi kutoka Shirikisho la Mpira Wa Miguu Afrika (CAF) pamoja na nchi washiriki waliofanikiwa kuingia katika fainali hiyo.
Fainali hizo zinahusisha timu nane zilizofanikiwa kufuzu na zitachuana kuweza kupata wawakilishi wawili kutoka katika kila kundi kwa ajili ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia la Vijana nchini Peru.Kwenye kupanga makundi hayo mwenyeji Tanzania ameangukia katika kundi la A akiwa na timu za Nigeria, Angola na Uganda.
Katika kundi B, kuna timu za Cameroon , Guinea, Morroco na Senegal.
Waangalizi kutoka CAF wameshakagua viwanja, mahospitali na hoteli kwa ajili ya timu zinazokuja nchini mwakani pamoja na waalikwa kutoka nchi mbalimbali.
Hivyo makala TANZANIA YAANGUKIA KUNDI A FAINALI ZA AFCON U17 MWAKANI
yaani makala yote TANZANIA YAANGUKIA KUNDI A FAINALI ZA AFCON U17 MWAKANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA YAANGUKIA KUNDI A FAINALI ZA AFCON U17 MWAKANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/tanzania-yaangukia-kundi-fainali-za.html
0 Response to "TANZANIA YAANGUKIA KUNDI A FAINALI ZA AFCON U17 MWAKANI"
Post a Comment