Loading...
title : UKARABATI KIWANDA CHA BUCO WASHIKA KASI
link : UKARABATI KIWANDA CHA BUCO WASHIKA KASI
UKARABATI KIWANDA CHA BUCO WASHIKA KASI
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akisaidiana na wahandisi na mafundi wa kikosi kazi cha kufufua kiwanda cha kubangua korosho cha Lindi (BUCO) kushusha kaangio la korosho ghafi kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati. Kiwanda cha BUCO kinafanyiwa ukarabati tayari kwa kuanza kubangua korosho zilizonunuliwa na serikali.
Fundi wa kurekebisha mashine za kubangua korosho Dastan Milanzi akifanya marekebisho ya mwisho kwenye moja ya mashine za kubangua korosho za kiwanda cha kubangua korosho cha Lindi (BUCO) kama alivyokutwa na mpiga picha wetu.
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya, akipata maelezo ya ukarabati wa mashine ya kubangua korosho kutoka kwa mratibu wa kikosi kazi cha kufufua kiwanda cha kubangua korosho cha Lindi (BUCO) Dkt. Isack Legonda (kushoto) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ukarabati wa kiwanda hicho kilichokabidhiwa kwa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Profesa Sylvster Mpanduji.
Baadhi ya wahandisi na mafundi wa kikosi kazi cha kufufua kiwanda cha kubangua korosho cha Lindi (BUCO) wakibeba kaangio la korosho ghafi. Kikosi kazi hicho kinatekeleza agizo alilolitoa wiki iliyopita Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Viwanda Vidogo (SIDO), Profesa Sylvester Mpanduji, akikagua shughuli za ubanguaji wa korosho unaofanywa na wabanguaji wadogo kwenye eneo la SIDO Mtwara. SIDO kwa kushirikiana na wajasriamali wadogo inatekeleza azma ya serikali kuhakikisha korosho zinabanguliwa nchini.
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya akishuhudia zoezi la kubangua korosho linalofanywa na wabanguaji wadogo kwenye eneo la SIDO mjini Mtwara. Mhandisi Manyanya yuko kwenye ziara ya kukagua uwezo wa viwanda vya kubangua korosho mikoa ya Mtwara na Lindi kujiridhisha kabla ya kuingia makubaliano ya kubangua korosho ya serikali. (Picha zote na Idara ya Habari-MAELEZO)
Hivyo makala UKARABATI KIWANDA CHA BUCO WASHIKA KASI
yaani makala yote UKARABATI KIWANDA CHA BUCO WASHIKA KASI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UKARABATI KIWANDA CHA BUCO WASHIKA KASI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/ukarabati-kiwanda-cha-buco-washika-kasi.html
0 Response to "UKARABATI KIWANDA CHA BUCO WASHIKA KASI"
Post a Comment