Loading...

Uongozi Wizara ya Viwanda Wawatoa Hofu Wakulima wa Korosho

Loading...
Uongozi Wizara ya Viwanda Wawatoa Hofu Wakulima wa Korosho - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Uongozi Wizara ya Viwanda Wawatoa Hofu Wakulima wa Korosho, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Uongozi Wizara ya Viwanda Wawatoa Hofu Wakulima wa Korosho
link : Uongozi Wizara ya Viwanda Wawatoa Hofu Wakulima wa Korosho

soma pia


Uongozi Wizara ya Viwanda Wawatoa Hofu Wakulima wa Korosho

Kuhakikisha azma ya Serikali ya Awamu ya Tano inanunua korosho yote ya wakulima inatimia kabla ya kipindi cha masika hakijashika kasi, uongozi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji umewatoa hofu wakulima wote wa mikoa ya kusini kuwa serikali inao uwezo wa kununua na kihifadhi korosho yote itakayonunuliwa.

Hakikisho hilo limetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchwaishaija wakati anahitimisha siku ya kwanza ya oparehseni ya ukaguzi wa maghala kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara. 
“Ziara ya ukaguzi wa maghala inatokana maagizo ya kikao cha tathmini ya Operesheni Korosho kilichoitishwa na Mwenyekiti wake Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga, ambapo pamoja na mambo mengine kilibaini ufinyu wa maeneo ya kuhifadhia korosho kutoka kwa wakulima” anasema Prof. Buchweishaija. 

Kwenye ziara hiyo Prof. Buchwaishaija pamoja na Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) Ludovick Nduhiye na maafisa wengine waandamizi wa wizara hiyo walifanikiwa kukagua maghala ya korosho kwenye wilaya za Mtwara, Mtama, Masasi na Nachingwea na kubaini kuwa maghala makuu na yale ya uhifadhi yana nafasi ya ziada kuhifadhi korosho zaidi ya tani elfu arobaini na nane.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji. Prof. Joseph Buchwaishaija (mwenye Kaunda suti), akisisitiza jambo kwa mwakilishi wa ghala la kuhifadhi korosho la OLAM Theophil Nandonde wakati alipofanya ziara ya kukagua maghala ya kuhifadhi korosho mikoa ya Mtwara na Lindi.
 Katibu Mkuu, Wizara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchwaishaija, akipokea maelezo kutoka kwa mwakilishi wa kampuni ya OLAM inayomiliki maghala ya kuhifadhi korosho eneo la bandari ya Mtwara. Pembeni ni Naibu Katibu Makuu wa Wizara hiyo sekta ya viwanda Bw. Ludovick Nduhiye. 
 Meneja wa Bandari Mkoa wa Mtwara, Bw. Abdulkarim  Salim akimueleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Joseph Buchwaishaija wakati wa ziara yake ya kukagua maghala ya kuhifadhi korosho kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi. Kwenye ziara hiyo Serikali imefanikiwa kupata nafasi ya ziada ya kuhifadhi korosho zaidi ya tani elfu arobaini na nane. 
Mwakilishi wa kiwanda cha kubangua korosho cha Sunshine kilichopo Mtama, Lindi akitoa ufafanuzi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Pof. Joseph Buchwaishaija alipotembelea kiwanda hicho ili kubaini uwezo wake wa kubangua korosho. (Picha na Idara ya Habari)

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala Uongozi Wizara ya Viwanda Wawatoa Hofu Wakulima wa Korosho

yaani makala yote Uongozi Wizara ya Viwanda Wawatoa Hofu Wakulima wa Korosho Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Uongozi Wizara ya Viwanda Wawatoa Hofu Wakulima wa Korosho mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/uongozi-wizara-ya-viwanda-wawatoa-hofu_3.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Uongozi Wizara ya Viwanda Wawatoa Hofu Wakulima wa Korosho"

Post a Comment

Loading...