Loading...

WABANGUAJI KOROSHO WAMPA KONGOLE RAIS MAGUFULI

Loading...
WABANGUAJI KOROSHO WAMPA KONGOLE RAIS MAGUFULI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WABANGUAJI KOROSHO WAMPA KONGOLE RAIS MAGUFULI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WABANGUAJI KOROSHO WAMPA KONGOLE RAIS MAGUFULI
link : WABANGUAJI KOROSHO WAMPA KONGOLE RAIS MAGUFULI

soma pia


WABANGUAJI KOROSHO WAMPA KONGOLE RAIS MAGUFULI


Uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kununua korosho za wakulima na kuzibangua nchini umepongezwa na Umoja wa Wabanguaji Wadogo wa Korosho Tanzania (UWWKT).

Akisoma risala mbele ya Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya, Mwenyekiti wa umoja huo Bi. Tumpale Magehema amesema uamuzi wa Rais Magufuli una nia ya kuwapa ajira wanachama wake wapatao 2881, jambo ambalo ni la kupongezwa.

Licha ya kutoa ajira Bi. Tumpale ameueleza uamuzi huo wa kijasiri uliofanywa na Rais Magufuli utaongeza ari ya kufanya kazi na kuchochea ukuaji wa uchumi hasa kwenye mikoa inayolima korosho kwa wingi.

Akitoa taarifa kwa mgeni rasmi, Katibu wa umoja huo Bw. Audax Mkongi, alimueleza mhandisi Manyaya kuwa umoja huo ni asasi mwamvuli ya kitaifa ya wabanguaji wadogo yenye jumla ya vikundi 183 kutoka wilaya tisa za mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Morogoro. Baadhi ya wilaya hizo ni Ulanga, Tandahimba, Kisarawe, Liwale na Ruangwa.

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya, akisisitiza jambo kwenye kikao na wawakilishi wa Umoja wa Wabanguaji Wadogo wa Korosho Tanzania(UWWKT) kilichofanyika kwenye hoteli ya Lindi Sea View. Pembeni ya Naibu Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, mhehsimiwa Shaibu Ndemanga, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Profesa Sylvester Mpanduji na kulia ni Mwenyekiti wa UWWKT Tumpale Magehema 
Baadhi ya wanachama wa Umoja wa Wabanguaji Wadogo wa Korosho Tanzania (UWWKT) wakimisikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, mhandisi Stella Manyanya. Umoja huo wa wabanguaji wadogo wa korosho umeonesha nia ya kubangua korosho iliyonunuliwa na serikali. 
Mwenyekiti wa Umoja wa Wabanguaji Wadogo wa Korosho Tanzania (UWWKT) Bi. Tumpale Magehema akisoma risala mbele ya Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, mhandisi Stella Manyanya alipofanya kikao na baadhi ya wanachama wa umoja huo mjini Lindi. 
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, mhandisi Stella Manyanya(katikati walioketi) kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa wanachama wa Umoja wa Wabanguaji Wadogo wa Korosho Tanzania (UWWKT). Wengine walioketi kuanzia kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Profesa Sylvester Mpanduji, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga, Mwenyekiti UWWKT Tumpale Magehema na Mkurugenzi Mtendaji wa ANSAF, Audax Rukonge. 



Hivyo makala WABANGUAJI KOROSHO WAMPA KONGOLE RAIS MAGUFULI

yaani makala yote WABANGUAJI KOROSHO WAMPA KONGOLE RAIS MAGUFULI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WABANGUAJI KOROSHO WAMPA KONGOLE RAIS MAGUFULI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/wabanguaji-korosho-wampa-kongole-rais.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WABANGUAJI KOROSHO WAMPA KONGOLE RAIS MAGUFULI"

Post a Comment

Loading...