Loading...
title : WABUNGE VITI MAALUMU WA VIPI TAFUTA VIKUNDI VYA AKINAMAMA JIMBO LA UKONGA.
link : WABUNGE VITI MAALUMU WA VIPI TAFUTA VIKUNDI VYA AKINAMAMA JIMBO LA UKONGA.
WABUNGE VITI MAALUMU WA VIPI TAFUTA VIKUNDI VYA AKINAMAMA JIMBO LA UKONGA.
Wabunge wa Viti maalumu mkoa wa Dar es salaam wakikabidhi Mashine za kupulizia dawa kwa kikundi cha wanawake cha Mzinga, wakwanza kushoto ni Mhe. Stella Ikupa, a naye fuatia ni Mhe. Mariam Kisangi a naye fuatia ni Ester Mhindi mwenyekiti kikundi cha Mzinga na wa mwisho kulia ni Mwenekiti wa Umoja wa wanawake( UWT Wilaya ya Ilala(Picha zote na John Luhende).
Na John Luhende
Mwambawahabari
Wabunge wa Viti maalumu mkoa wa Dar es salaam, wametakiwa kufanyakazi karibu na wananchi hasa kusaidia vikundi vya akinamama wanaofanya kazi zakujiongezea kipato ikiwemo ujasiliamali na ukulima wa mbogamboga.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Wilaya ya Ilala Amina Dodi,wakati wa ziara ya wabunge wa wa viti Maalumu katika kata za Kitunda ,Mzinga ,na Majohe,ambapo wabunge hao wametoa msaa wa fedha , pembejeo za kilimo na cherehani kwa vikundi vya akina mama.
“Katika kipindi cha uongozi wangu nimejitahidi sana kuwahamasisha wabunge wetu kuwa karibu na wananchi na wabunge hawa wamekubali kushuka chini kabisa na kukutana na wanawake wameona shida zao na wameguswa na kuona umuhimu wa kusaidia vikundi hivi wametimiza ahadi zao “Alisema
Aidha Mama Dodi amevitaka vikundi vyote vilivyopatiwa msaada ,kuwa na umoja , Upendo na mshikamano na kuvitumia vifaana fedha walizo pewa kama kikundi na kuacha ubinafisi kutokubali mtu yeyote kuwavuruga na kuinuka kutaka kuhodhi mali za kikundi.
Wabunge wa viti maalumu mkoa wa Dar es salaam,ambao ni Mariam Kisangi , Stella Ikupa, na Angela Kairuki, kwa kushirikiana wakiwa katika kampeni za Ubunge Jimbo la Ukonga waliahidi kuvisaidia vikundi hivyo ,ambapo katika kikundi cha Winners wametoa cherehani moja kuwezesha kikundi cha wananwake wanoa saidi kundi la wasichana 11 wanaoishi mazingira magumu,walipata mimba za utotoni na wanalea watoto wao, kikundi kingine ni Tufashane group kina watu 30,nashughulika na ulimaji wa mboga boga ambao nao wamepewa fedha shilingi 500,000.
Vikundi vingine vilivyo saidiwa ni pamoja na Mzinga group ,chenye watu 30 kinajishughulisha na ukulima wa Mbogamboga , kimesaidiwa mashine 4 za kupulizia dawa za kuuwa wadudu,na kituo chaTaarifa na Maarifa Kitunda ambacho kimepatiwa shilingi 500,000 kwaajili ya pembejeo za kilimo na kununua mashine za kumwagilia bustani.
Kwaupande wake Mbunge Mariam Kisangi amesema ,wabunge wa Chama cha Mapinduzi wakiahidi wanatimiza na wao waliahidi kuvisaidia vikundi hivyo na ameupongeza uongozi wa UWT wilaya yaIlala na kata za kitunda na Majohe kwa uongozi bora na kuendelea kuhamasisha wanawake,huku akiwashukuru wote waliopiga kura kumchagua mbunge Mwita Waitara na kusema kuwa hapo mwanzo walishindwa kuja kwakuwa Mbuge vitimaalumu hawezi kuingia jimboni hadi aombe ruhusa ya Mbunge wa jimbo,nasasa wanaweza kuingia jimboni humo kwa kuwa Waitara ni mwenzao anawaruhusu.
“Kama kunakata ngumu wakati wa uchaguzi ilikuwa ni kitunda lakini tuna washukuru ninyi akinamama hamkutuangusha katika uchaguzi na mmechagua Chama cha Mapinduzi na sisi tuna washukuru na sisi katika harakati zile tuliahidi kuwa saidi katika shughuli zenuna leotumetimiza ahadi yetu kwa vikundi tuoliwaahidi ”Alisema.
Naye Mbuge Stella Ikupa ambaye pia ni Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na wenyeulemavu, amewataka akinamama hao kuwa na umoja ,na chukhangamkia fursa za mikopo ya wanawake inayotolewa na Halmashauri ambayo haina riba endeleeni kuhamisisha na wanawake wengine.
“Ninyi na sisi tayari tumejenga udugu wa damu hakuna anaye weza kuuvunja,naomba muendelee kutuamini chama cha Mapinduzi tunatimiza hatayale ambayo yalikuwa yana onekana magumu yanatekelezwa Rais Magufuli alipo ingia madaraka ni mwezi mmoja baada ya kuingia madarakani Elimu ilianza kutolewa bure na sasa tumeona amenunua ndege, hatuwezi kutekeleza yote kwa sikumoja lakini pale ambacho kinapatika kidogo tutajitahidi kukigawa angalau kila mmoja kiweze kumfikia”Alisema.
Kwa upande wa vikundi vya wanawake vilivyo patiwa msaada huo kwa pamoja wamewashukuru wabunge hao na kusema kuwa haaamini kilicho tokea na wamefurahi na kuwapongeza wabunge hao kwa kuwakumbuka na kuwapatia msaada huo .
“Niwachache wenye moyo huo tuna shukuru mno tuidhani wanaomba kura tu hawatatimiza ahadi sasa leo tumeona na tumepokea Mungu awazidishie Tulikuwa tuna simangwa tukienda kuazima mashine na sasa tumepata zakwetu“Alisema Ester Mhindi mwenyekiti kikundi cha Mzinga.
Hatahivyo vikundi hivyo bado vinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa mashine za kushona,ambapo viongozi wao wameomba wadau mbalimbali kuendelea kuviwezesha.
Hivyo makala WABUNGE VITI MAALUMU WA VIPI TAFUTA VIKUNDI VYA AKINAMAMA JIMBO LA UKONGA.
yaani makala yote WABUNGE VITI MAALUMU WA VIPI TAFUTA VIKUNDI VYA AKINAMAMA JIMBO LA UKONGA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WABUNGE VITI MAALUMU WA VIPI TAFUTA VIKUNDI VYA AKINAMAMA JIMBO LA UKONGA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/wabunge-viti-maalumu-wa-vipi-tafuta.html
0 Response to "WABUNGE VITI MAALUMU WA VIPI TAFUTA VIKUNDI VYA AKINAMAMA JIMBO LA UKONGA."
Post a Comment