Loading...
title : WAJASIRIAMALI 25,000 MKOANI TABORA WAANZA KUGAWIWA VITAMBULISHO VYA RAIS MAGUFULI
link : WAJASIRIAMALI 25,000 MKOANI TABORA WAANZA KUGAWIWA VITAMBULISHO VYA RAIS MAGUFULI
WAJASIRIAMALI 25,000 MKOANI TABORA WAANZA KUGAWIWA VITAMBULISHO VYA RAIS MAGUFULI
Na Tiganya Vincent, Tabora
WAJASIRIAMALI wadogo wadogo mkoani Tabora wameonywa kutotumia vitambulisho walivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuuzia biashara za wafanyabiashara wakubwa na hivyo kuwa chanzo cha ukwepeji kodi.
Onyo hilo limetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akigawa vitambulisho 25,000 kwa Wakuu wa Wilaya saba za Mkoa huo na viongozi watatu wa Wajasiriamali wa Manispaa ya Tabora ikiwa ni uzinduzi wa zoezi hilo mkoani humo.
Alisema vitambulisho vilivyotolewa na Rais ni kwa ajili ya Wajasiriamali wadogo wadogo na sio vinginevyo na ambao ni wale biashara zao kwa siku zote 365 za mwaka mapato yao hayazidi shilingi milioni nne.
Mwanri alisema ni kosa kuazimisha kitambulisho au kubeba bidhaa za wafanyabiashara wakubwa na kuongeza kuwa atakayebainika atakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya Sheria ili achukuliwe hatua.
Aidha alisema Mkoa huo ulipatiwa vitambulisho 25,000 vilivyotolewa na Rais Magufuli hivi karibuni ambapo vimegawanywa kwa Halmashauri zote nane za Mkoa wa Tabora na kila moja imepata vitambulisho 3125.
Maandamano maalumu ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwatambua rasmi ya kuwapatia vitambulisho yaliyoandaliwa na Wajasiriamali wa Manispaa ya Tabora yakiingia kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora tayari kwa kugawiwa vitambulisho.
Baadhi ya Wajasiriamali wa Manispaa ya Tabora na viongozi mbalimbali wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha) kabla ya kuanza kugawa vitambulisho vilivyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya Wajasiriamali.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akimvisha kitambulisho Katibu Msaidizi wa Wajasiriamali Manispaa ya Tabora Ashura Rashid baada ya aaandamano maalumu ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwatambua rasmi ya kuwapatia vitambulisho yaliyoandaliwa na Wajasiriamali wa Manispaa ya Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (wenye Tshirt ya Njano) akimkabidhi vitambulisho 6250 Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula (kushoto) kwa ajili kwenda kuwagawia Wajasiriamali wilayani kwake. Picha na Tiganya Vincent
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAJASIRIAMALI 25,000 MKOANI TABORA WAANZA KUGAWIWA VITAMBULISHO VYA RAIS MAGUFULI
yaani makala yote WAJASIRIAMALI 25,000 MKOANI TABORA WAANZA KUGAWIWA VITAMBULISHO VYA RAIS MAGUFULI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAJASIRIAMALI 25,000 MKOANI TABORA WAANZA KUGAWIWA VITAMBULISHO VYA RAIS MAGUFULI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/wajasiriamali-25000-mkoani-tabora.html
0 Response to "WAJASIRIAMALI 25,000 MKOANI TABORA WAANZA KUGAWIWA VITAMBULISHO VYA RAIS MAGUFULI"
Post a Comment