Loading...

WALIOSOMA SHULE YA MSINGI MWANGA KUANZIA MWAKA 1958 WAJIPANGA KUCHANGIA MIUNDOMBINU SHULENI HAPO

Loading...
WALIOSOMA SHULE YA MSINGI MWANGA KUANZIA MWAKA 1958 WAJIPANGA KUCHANGIA MIUNDOMBINU SHULENI HAPO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WALIOSOMA SHULE YA MSINGI MWANGA KUANZIA MWAKA 1958 WAJIPANGA KUCHANGIA MIUNDOMBINU SHULENI HAPO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WALIOSOMA SHULE YA MSINGI MWANGA KUANZIA MWAKA 1958 WAJIPANGA KUCHANGIA MIUNDOMBINU SHULENI HAPO
link : WALIOSOMA SHULE YA MSINGI MWANGA KUANZIA MWAKA 1958 WAJIPANGA KUCHANGIA MIUNDOMBINU SHULENI HAPO

soma pia


WALIOSOMA SHULE YA MSINGI MWANGA KUANZIA MWAKA 1958 WAJIPANGA KUCHANGIA MIUNDOMBINU SHULENI HAPO

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

WANAFUNZI waliosoma Shule ya Msingi ya Mwanga, mkoani Kilimanjaro kuanzia mwaka 1958 wanatarjiwa kushiriki tamasha la kuchangia uboreshaji wa miundombinu mbalimbali shuleni hapo litakalofanyika Desemba 27 mwaka huu.

Ushiriki wa wanafunzi hao ni matokeo ya ombi la mwalimu mkuu wa shule hiyo Christina Lyari la kuwaomba wananchi, wadau na wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kujitokeza katika tamasha hilo la aina yake.

Lyari alisema wakati umefika kwa kila aliyepita shule hiyo kurudisha fadhili kwa kusaidia kuboresha miundombinu.“Tunahitaji kukarabati majengo kama ofisi ya walimu, maktaba, choo cha walimu, uwekaji wa madirisha ya aluminiamu na kununua komputa na viongine vingi hivyo ujio wanamwanga ni muhimu,” alisema.

Aidha Mwalimu Lyari alisema amefikia hatua hiyo baada ya kubaini kuwa shule hiyo imetengeneza viongozi, wataalam, watafiti, wanasiasa na wajasiriamali wengi wanaoweza kutatua changamoto nyingi zilizopo kama wakishirikishwa ipasavyo .Akizungumzia ziara hiyo mmoja wa wahitimu wa Shule ya Msingi Mwanga na aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW), Dk. Abu Mvungi alisema wameamua kufanya ziara hiyo kama moja ya sehemu ya kuonesha walipotoka.

“Nampongeza mwalimu kwa kuonyesha moyo wa dhati, ushirikiano na ushirikishaji wa katika suala zima la kutumikia jamii, suala hili lina umuhimu mkubwa na linahitaji kuungwa mkono na kuendelezwa na sisi tutamuunga mkonon kwani Mwanga ndio mwanga wetu,” alisema.

Alisema shule hiyo ni mkombozi wa maisha yake hivyo hawezi kuisahau hivyo kuwataka wale wote waliosoma Shule ya Msingi Mwanga kujitokeza.
Kwa upande wake Mhasibu Mkuu wa Wakala wa Barabara mkoa wa Dar es Salaam (Tanroads), Haruni Msuya alisema hawezi kuisahau shule hiyo kwani ndio msingi unaomwezesha kuendelea kuitumikia jamii 

Wengine waliosoma shule hiyo ni Profesa Abdulkareem Mruma, Daktari Bingwa Hospitali ya Rufaa Mbeya, Omary Salehe, Mliki wa Mabasi ya Chakito, Meraji Kidundi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Richard Mziray na wengine wengi.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mwanga mkoani Kilimanjaro Christina Lyari akionesha mazingira ya shule hiyo ambayo wanafunzi waliosoma hapo kuanzia mwaka 1958 wanatarajia kushiriki tamasha la kuchangia fedha kwa akili ya uboreshaji wa miundombinu ya shule hiyo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwanga Christina Lyari akiwa ofisini kwake


Hivyo makala WALIOSOMA SHULE YA MSINGI MWANGA KUANZIA MWAKA 1958 WAJIPANGA KUCHANGIA MIUNDOMBINU SHULENI HAPO

yaani makala yote WALIOSOMA SHULE YA MSINGI MWANGA KUANZIA MWAKA 1958 WAJIPANGA KUCHANGIA MIUNDOMBINU SHULENI HAPO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WALIOSOMA SHULE YA MSINGI MWANGA KUANZIA MWAKA 1958 WAJIPANGA KUCHANGIA MIUNDOMBINU SHULENI HAPO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/waliosoma-shule-ya-msingi-mwanga.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WALIOSOMA SHULE YA MSINGI MWANGA KUANZIA MWAKA 1958 WAJIPANGA KUCHANGIA MIUNDOMBINU SHULENI HAPO"

Post a Comment

Loading...