Loading...

Wananchi zaidi ya Milioni 4 Dar kupatiwa Kingatiba dhidi Matende na Mabusha

Loading...
Wananchi zaidi ya Milioni 4 Dar kupatiwa Kingatiba dhidi Matende na Mabusha - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wananchi zaidi ya Milioni 4 Dar kupatiwa Kingatiba dhidi Matende na Mabusha, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wananchi zaidi ya Milioni 4 Dar kupatiwa Kingatiba dhidi Matende na Mabusha
link : Wananchi zaidi ya Milioni 4 Dar kupatiwa Kingatiba dhidi Matende na Mabusha

soma pia


Wananchi zaidi ya Milioni 4 Dar kupatiwa Kingatiba dhidi Matende na Mabusha


NA WAMJW, DAR ES SALAAM

WAKAZI wa Dar es Salaam wapatao Milioni 4.3 wanatarajiwa kumeza Kingatiba dhidi ya magonjwa ya matende na mabusha (Ngirimaji) pamoja na minyoo ya tumbo, kuanzia Disemba 15 hadi 20, mwaka huu.

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele (NTD), Dkt. Upendo Mwingira wakati wa Warsha ya Wanahabari kuhusu magonjwa hayo hapa nchini.

Dkt. Upendo Mwingira amewataka wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo kwani kingatiba hiyo itatolewa bila malipo katika maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam.“Hii sio chanjo. Ni kijngatiba na zoezi hili linaenda kumkinga mtu dhidi ya magonjwa ya mabusha na matende pamoja na minyoo na itatolewa kuanzia umri wa miaka 5 na kuendelea” Amasema Dkt.Upendo Mwingira.

Ameongeza kuwa, “Wananchi watakaojitokeza watamezeshwa kingatiba hizo papohapo na zoezi hili utolewa kila mwaka mara moja” amebainisha.
Magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele ni pamoja na Usubi,Vikope (Trakoma), Matende, Mabusha (Ngirimaji), na Minyoo ya tumbo.

Zoezi hilo la ugawaji wa dawa litatekelezwa katika vituo vyote vya Afya, Zahanati,Hospitali, sokoni,vituo vya usafiri,pamoja na Ofisi za Serikali, maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi na Mashirika ya Umma na hivyo wananchi wanaombwa kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo ambayo haina malipo yoyote.
Mratibu wa Haifa wa Mpan go wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kutoka Wizara ya Afya Dkt.Upendo Mwingira akitoa ufafanuzi kuhusu zoezi la umezeshaji wa Kinga Tiba za matende na mabusha(ngirimaji ) kwenye warsha ya waandishi wa habari iliyofanyika ofisi ndogo za wizara zilizopo Jijini Dar es salaam
Afisa Mpango Oscar Kaitaba akiwaonesha Kinga tiba hizo waandishi wa habari(hawapo pichani).Zoezi la umezeshaji kwa Mkoa wa Dar es Salaam linalotarajiwa kuanza disemba 15 hadi 20 mwaka huu
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali ,Wziara ya Afya Catherine Sungura akiongea na waandishi wa Habari wakati ya warsha hiyo kulia ni afisa Mawasiliano kutoka kitengo cha Elimu ya Afya kwa Umma Said Makora Waandishi wa Habari walioshiri warsha ya umezeshaji Kinga tiba kwa Mkoa wa Dar es Salam iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi Mdogo za wizara zilizopo Jijini Dar es salaam
Baadhi ya wandishi wakifuatilia mada katika semina hiyo.
Waandiahinwa Habari walioshiri warsha ya umezeshaji Kinga tiba kwa Mkoa wa Dar es Salam iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi Mdogo za wizara zilizopo Jijini Dar es salaam



Hivyo makala Wananchi zaidi ya Milioni 4 Dar kupatiwa Kingatiba dhidi Matende na Mabusha

yaani makala yote Wananchi zaidi ya Milioni 4 Dar kupatiwa Kingatiba dhidi Matende na Mabusha Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wananchi zaidi ya Milioni 4 Dar kupatiwa Kingatiba dhidi Matende na Mabusha mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/wananchi-zaidi-ya-milioni-4-dar.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wananchi zaidi ya Milioni 4 Dar kupatiwa Kingatiba dhidi Matende na Mabusha"

Post a Comment

Loading...