Loading...
title : WATENDAJI DODOMA WATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KUVUTIA ZAIDI WAWEKEZAJI
link : WATENDAJI DODOMA WATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KUVUTIA ZAIDI WAWEKEZAJI
WATENDAJI DODOMA WATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KUVUTIA ZAIDI WAWEKEZAJI
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge amewataka watendaji wa Mkoa wa Dodoma kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kujenga mazingira rafiki na kuboresha mazingira ya biashara.
Ametoa kauli hiyo leo wakati akifungua kikao kazi cha siku moja cha Baraza La Biashara Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili Mwongozo wa Uwekezaji mkoani humo Desemba 21, 2018 katika Chuo cha Mipango.Dkt.Mahenge aliwataka watendaji kuzingatia utendaji wenye weledi, tija na unaovutia wawekezaji kuwekeza mkoani humo kwa kuzingatia kuwa ndiyo Makao Makuu ya Nchi.“lazima utendaji wetu uwe wa namna bora na upekee katika kuweza kuvutia wawekezaji kwa kuwa na miundombinu rafiki ya biashara na kutatua changamoto zozote zinazoweza kuwakwamisha wawekezaji”.Alieleza Dkt.Mahenge.
Aliongeza kuwa, Halmashauri zote zione umuhimu wa kuboresho mazingira ya uwekezaji na kutumia fursa zilizopo katika kufikia malengo ya kujenga uchumi endelevu.“Nivyema sasa kila Halmashauri ikaona fursa na kuzitumia ikiwemo zile za kifedha na kuhusisha taasisi za kifedha ikiwemo Mabenki ili kuona kila lengo linafikiwa na kuwa na uwekezaji wenye tija nchini”.alisisitiza Dkt.Mahenge
Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi alieleza umuhimu wa kuzitumia fursa zilizopo Dodoma na kuwa na uwekezaji wenye tija kwa kila eneo kwa kuzingatia mazingira yaliyopo.
“Lazima fursa zilizopo Dodoma zitumike kwa malengo yenye tija kwa kuhakikisha mkoa unabaki kuwa kivutio cha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ,”Alieleza Kunambi.Aliongeza kuwa Jiji hilo limetenga maeneo mbalimbali ya uwekezaji na kuyapima kulingana na mahitaji ya uwekezaji ikiwemo ya viwanda, Biashara na makazi.Kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kimefayika ili kupitia muongozo wa uwekezaji katika mkoa wa huo hali itakayochochea uwekezaji na kukuza uchumi na kuchochea maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge akifungua kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Muwakilishi wa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara Bw. Patrick Mavika akizungumza wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Wajumbe wa Baraza la Biashara la mkoa wa Dodoma wakifuatilia kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Bw. Godwin Kunambi akizungumzia fursa zilizopo katika Jiji Dodoma wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) Bw. Mussa Martine akiwasilisha mada wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.
Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe akizungumza wakati wa kikao kazi cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Dodoma kilicholenga kujadili na kutoa maoni kuhusu muongozo wa uwekezaji katika mkoa huo leo jijini humo.(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Hivyo makala WATENDAJI DODOMA WATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KUVUTIA ZAIDI WAWEKEZAJI
yaani makala yote WATENDAJI DODOMA WATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KUVUTIA ZAIDI WAWEKEZAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATENDAJI DODOMA WATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KUVUTIA ZAIDI WAWEKEZAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/watendaji-dodoma-watakiwa-kuweka.html
0 Response to "WATENDAJI DODOMA WATAKIWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KUVUTIA ZAIDI WAWEKEZAJI"
Post a Comment