Loading...
title : WAZIRI MKUU AZINDUA TAWI LA BENKI YA CRDB RUANGWA
link : WAZIRI MKUU AZINDUA TAWI LA BENKI YA CRDB RUANGWA
WAZIRI MKUU AZINDUA TAWI LA BENKI YA CRDB RUANGWA
*Asema litahamasisha ukuaji wa uchumi na wananchi watahifadhi fedha zao
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezindua tawi la benki ya CRDB wilayani Ruangwa na kuushukuru uongozi wa benki hiyo kwa kuwa tawi hilo litahamasisha ukuaji wa uchumi pamoja na kuwawezesha wananchi kujua umuhimu wa kuhifadhi fedha zao benki.
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema ni vema kwa benki ya CRDB ikasogeza huduma hususan kwa wananchi waishio katika miji mikubwa iliyo mbali na makao makuu ya wilaya kwa kufungua ofisi za uwakala na kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Desemba 31, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ruangwa mara baada ya kuzindua tawi la benki ya CRDB, ambapo ametumia fursa hiyo kuwahamisha wananchi kutumia benki kwa kuhifadhi fedha zao.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kwa sasa benki hiyo inatakiwa itoe mikopo midogo, ya kati na mikubwa kulingana na uhitaji wa wajasiriamali ndani ya wilaya hiyo kwa sababu mikopo itawawezesha wananchi waweze kukuza mitaji na kujikwamua kiuchumi. Pia Waziri Mkuu ameipongeza benki ya CRDB kwa kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli katika kuboresha maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo za afya pamoja na elimu kupitia misaada mbalimbali inayotolewa na benki hiyo nchini.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema benki ya CRDB imekua na kupanua wigo wake wa kufikisha huduma kwa wateja na kuunga mkono sera ya Serikali ya kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata huduma za fedha.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kushoto ni Mkewe Mary, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay, wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ruangwa, Hashim Ngandirwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Wengine pichani kutoka kulia ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kushoto ni mkewe Mary, wapili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Jengo la Benki ya CRDB tawi la Ruangwa ambalo lilizinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Desemba 31, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi kompyuta mpakato Kiongozi wa Chama cha Msingi cha Umoja 2017, Omari Hassani Magoma baada ya kuzindua tawi la Benki hiyo la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kompyuta Mpakato 28 zilitolewa na Benki ya CRDB kwa Vyama vya Ushirika vya Msingi wilayani Ruangwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya CRDB, Ally Hussein Laay na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Kiongozi wa Chama cha Msingi cha Umoja 2017 wilayani Ruangwa, Omari Hassan Magoma akionyesha Kompyuta Mpakato aliyokabidhiwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati Waziri Mkuu alipozindua tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Kompyuta mpakato 28 zilitolewa na Benki ya CRDB kwa vyama vya Ushirika vya Msingi (AMCOS) wilayani Ruangwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Ally Hussein Laay na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela.
Waalikwa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kuzindua Tawi la Benki ya CRDB la Ruangwa, Desemba 31, 2018. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu .
Hivyo makala WAZIRI MKUU AZINDUA TAWI LA BENKI YA CRDB RUANGWA
yaani makala yote WAZIRI MKUU AZINDUA TAWI LA BENKI YA CRDB RUANGWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU AZINDUA TAWI LA BENKI YA CRDB RUANGWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/12/waziri-mkuu-azindua-tawi-la-benki-ya.html
0 Response to "WAZIRI MKUU AZINDUA TAWI LA BENKI YA CRDB RUANGWA"
Post a Comment