Loading...

AJIFUNGUA AKIWA MAHUTUTI KWA MIAKA 10

Loading...
AJIFUNGUA AKIWA MAHUTUTI KWA MIAKA 10 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AJIFUNGUA AKIWA MAHUTUTI KWA MIAKA 10, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AJIFUNGUA AKIWA MAHUTUTI KWA MIAKA 10
link : AJIFUNGUA AKIWA MAHUTUTI KWA MIAKA 10

soma pia


AJIFUNGUA AKIWA MAHUTUTI KWA MIAKA 10

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii

NCHINI Marekani, Mjini Phoenix katika kliniki ya shirika la afya la Hacienda mwanamke mmoja aliyekaa mahututi (Koma) kwa miaka 10 amejifungua mtoto wa kiume katika kliniki hiyo.

Shirika la utangazaji la CNN nchini humo limeripoti kuwa Disemba 29 mwanamke huyo ambaye hakujulikana kama mjamzito hadi alipoonesha dalili za kujifungua, alijifungua mtoto wa kiume na polisi wa wameanza uchunguzi kwa udharilishwaji huo wa kingono kwa kutaka vipimo kwa damu (DNA) kwa wanaume  wanaofanya kazi kituoni hapo na taarifa iliyotolewa siku ya Ijumaa na Sajent. Tommy Thomson ilisema kuwa uchunguzi bado unaendelea.

Imeelezwa kuwa mwanamke huyo ambaye jina lake halikutajwa kwa kuwa amedharilishwa kingono alikaa kituoni hapo kwa muda mrefu katika kituo hicho cha Hacienda akipatiwa matibabu baada ya kupata tatizo hilo miaka 14 iliyopita.

Aidha imeelezwa kuwa hali ya mtoto aliyezaliwa ni njema kabisa na ulinzi katika kituo hicho umeimarishwa hasa kwa wanaume ambapo hawaruhusiwi kuingia Hacienda bila kuambatana na wasaidizi wakike.

Kliniki hiyo imelaani vikali tukio hilo na tayari mkurugenzi mkuu Bill Timmons ameachia madaraka mapema Jumatatu.

Hacienda ni kliniki maarufu nchini Marekani kwa kuhudumia watu wenye magonjwa sugu, watoto wachanga na watu wenye ulemavu.


Hivyo makala AJIFUNGUA AKIWA MAHUTUTI KWA MIAKA 10

yaani makala yote AJIFUNGUA AKIWA MAHUTUTI KWA MIAKA 10 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AJIFUNGUA AKIWA MAHUTUTI KWA MIAKA 10 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/ajifungua-akiwa-mahututi-kwa-miaka-10.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "AJIFUNGUA AKIWA MAHUTUTI KWA MIAKA 10"

Post a Comment

Loading...