Loading...

Benki M Tanzania PLC yashindwa kujiendesha , yahamishiwa Azania Benki Limited.

Loading...
Benki M Tanzania PLC yashindwa kujiendesha , yahamishiwa Azania Benki Limited. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Benki M Tanzania PLC yashindwa kujiendesha , yahamishiwa Azania Benki Limited., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Benki M Tanzania PLC yashindwa kujiendesha , yahamishiwa Azania Benki Limited.
link : Benki M Tanzania PLC yashindwa kujiendesha , yahamishiwa Azania Benki Limited.

soma pia


Benki M Tanzania PLC yashindwa kujiendesha , yahamishiwa Azania Benki Limited.

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imeihamishia Benki M Tanzania PLC kwenda Azania Benki limited baada ya kubaini kuwa na upungufu wa ukwasi na kutoa huduma kwa wateja.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Benard Kibesse alisema kuwa Benki kuu imechukua uamuzi huo wa kuhamisha mali na madeni ya Benki M kwenda Azani benki ili kuwezesha taasisi za kifedha kufanya kazi na kuwa imara zaidi kwa kujifunza kupitia benki M.
“Kwa mamlaka iliyopewa Benki Kuu ya Tanzania chini ya sheria kifungu 58(2) cha sheria za mabenki na taasisi za fedha yay a mwaka 2006, Benki Kuu imeamua kuchukua jukumu hili ili kuweza kulinda maslahi ya wateja wenye amana katika benki M Tanzania PLC”, Alisema Gavana Msaidizi wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Benard Kibesse
Dkt. Kibesse alisema kuwa kwa sasa Benki Kuu ya Tanzania, Azania Benki Limited na wadau wengine wa taasisi za kifedha wako kwenye mchakato wa mwisho wa kisheria  kuhusu kukamilisha uhamishaji wa mali na madeni ya Benki M kwenda Azania Benki Limited na mchakato utakapokamilika Benki ya Azania utaujulisha umma kuhusu mchakato huo.
Aidha Dkt. Kibesse aliongeza kuwa mchakato huo hauendani na kusitishwa kwa marejesho ya mikopo kwa wateja wa Benki M walioingia mkataba na kukopa kwenye benki ya kwamba wanapaswa waendelee kurejesha mikopo hiyo na wanatakiwa kulipa ndani ya siku 7 tu.
“Wateja wote wenye mikopo wanatakiwa waendelee kulipa mikopo yao kulingana na mikataba yao waliyoingia na Benki M Tanzania PLC”, Alisisitiza Dkt. Kibesse.
Benki M ilianzishwa na kupewa leseni ya shughuli za kibenki hapa Tanzania mwaka 2008 na ilikuwa moja ya benki imara iliyokuza mtaji hadi kufikia fedha za kitanzania shilingi trilioni 1 na kugawanyika katika matawi matano huku matawi makuu matatu yakiwa Jijini Dar es Salaam na mengine Mwanza pamoja na Arusha matawi ambayo yalilegalega mnamo mwaka 2018.
Tangu Tarehe 2 Agosti 2018 Benki Kuu ya Tanzania iliamua kuchukua jukumu la usimamizi kwa Benki M baada ya kubaini benki hii kushindwa kulipa madeni yake ikiwemo amana za wateja wake, pia Dkt.Kibesse amewahakikishia wadau wanaotumia huduma za kifedha kuwa Benki Kuu ya Tanzania itaendelea kulinda maslahi yao pamoja na uhimilifu katika Sekta ya Fedha nchini.
MWISHO


Hivyo makala Benki M Tanzania PLC yashindwa kujiendesha , yahamishiwa Azania Benki Limited.

yaani makala yote Benki M Tanzania PLC yashindwa kujiendesha , yahamishiwa Azania Benki Limited. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Benki M Tanzania PLC yashindwa kujiendesha , yahamishiwa Azania Benki Limited. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/benki-m-tanzania-plc-yashindwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Benki M Tanzania PLC yashindwa kujiendesha , yahamishiwa Azania Benki Limited."

Post a Comment

Loading...