Loading...
title : BITEKO AKALIPIA AJALI MAENEO YA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI
link : BITEKO AKALIPIA AJALI MAENEO YA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI
BITEKO AKALIPIA AJALI MAENEO YA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI
Na, Nuru Mwasampeta
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko amewataka wachimbaji wadogo wa madini kuzingatia uchimbaji salama ili kuepusha ajali zinazotokea mara kwa mara katika maeneo ya migodi. Ametanabaisha kuwa akifa mtanzania mmoja huyo Mtanzania ni muhimu kuliko mgodi wote, ‘kuliko mtanzania mmoja afe ni bora huo mgodi usiwepo’.
Aliyasema hayo leo tarehe 04 mwezi Januari alipokuwa akifungua mafunzo ya wachimbaji wadogo katika eneo la uchimbaji mji wa Buhemba wilayani Butiama mkoani Mara inayoendelea kwa siku mbili.
Biteko alibainisha kuwa, Buhemba ni eneo linaloongoza kwa ajali kwenye migodi, huu mgodi ulifungwa na toka umefunguliwa kuna vifo vya wachimbaji kumi na mbili na majeruhi 20, Serikali haiwezi ikakubali hali hiyo iendelee “Mimi nakwambia mwenyekiti sitakubali hali hii iendelee mimi mwenyewe nitakuja kuufunga tena mgodi huu kama hali hiyo itaendelea hatuwezi kupoteza maisha ya watanzania” Biteko alisisitiza.
Biteko aliongeza kwa kusema, Serikali haiko tayari kuona kuwa watu wanaendelea kufa ndio maana imeamua kufika na kuandaa mafunzo kwa ajili ya wachimbaji wadogo ili waweze kufundishwa namna bora za uchimbaji salama na wenye tija. Biteko alisema mafunzo hayo yanalenga kuwafundisha wachimbaji wadogo masuala ya uchimbaji salama, uchenjuaji, afya, na mazingira ya uchimbaji katika mkoa huu wa Mara.
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi (aliyesimama) akieleza jambo mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (Kushoto) alipofika ofisini kwake kuelezea uwepo wake katika wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza jambo mbele ya wachimbaji wadogo waliohudhuria mafunzo ya namna bora ya kuboresha uchimbaji wao yanayofanyika katika Wilaya ya Butiama Mkoani Mara.
Baadhi ya Wachimbaji wadogo waliohudhuria mafunzo yaliyoandaliwa kwa ajili yao yenye lengo la kuboresha sekta ya uchimbaji mdogo wa Madini yanayoendelea katika wilaya ya Butiama mjini Buhemba mkoani Mara.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (aliyekaa kushota) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini waliohudhuria mafunzo ya namna bora ya kujikita katika uchimbaji wenye tija.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Hivyo makala BITEKO AKALIPIA AJALI MAENEO YA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI
yaani makala yote BITEKO AKALIPIA AJALI MAENEO YA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BITEKO AKALIPIA AJALI MAENEO YA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2019/01/biteko-akalipia-ajali-maeneo-ya.html
0 Response to "BITEKO AKALIPIA AJALI MAENEO YA WACHIMBAJI WADOGO WA MADINI"
Post a Comment